Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Malipo ya Tasaf kufanyika kielektroniki
Habari Mchanganyiko

Malipo ya Tasaf kufanyika kielektroniki

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Robert Masunya
Spread the love

JOSEPHINE Joseph, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf amesema, malipo ya walengwa wa kaya masikini awamu ya pili yatafanyika kwa njia ya kielektroniki. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema walengwa watakuwa wanalipwa fedha zao kupitia mitandao ya simu na benki ili kuondoa walengwa hewa.

Josephine amesema hayo jana Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mafunzo ya kujenga uelewa kwa ma Ofisa Ugani wa Halmashauri wa Wilaya ya Iringa.

Alisema wanatakiwa kufanya uhakiki kwa weledi ili kuondoa malalamiko ya awamu iliyopita kuonekana ina walengwa wengi hewa.

“Kuna mfumo ambao tumeutengeneza kwa kushirikiana na wizara ya fedha, mlengwa atakuwa analipwa kupitia mawakala wa simu au benki kwa kutumia kitambulisho cha Nida, ama namba ya nida kwa wale ambao itashindikana kabisa kuwa na akaunti benki au simu watalipwa kupitia mawakala wa simu au benki,” alisema.

Alisema wanahitaji ushirikiano mkubwa kutoka Nida ili walengwa wapate kitambulisho au namba ili kuwasaidia walengwa wote kwa sababu ndio zitatumika kumtambua mlengwa kabla ya kupokea malipo.

Josephine alisema jina litakalosajiliwa katika orodha ya kaya masikini ndio litakalotumika kupokea fedha kwa kutumia kitambulisho cha Nida.

“Tunataka kuwa na orodha halisi ya walengwa kwenye masijala ya kaya za walengwa ambao wamefariki, ambao walikuwa ni kaya ya mtu mmoja asiye na tegemezi, kaya ambayo imehama, kaya ya kiongozi wa vijiji, msimamizi wa jamii, kaya ambayo haikufika kuchukua malipo yake mara mbili mfululizo kaya hizo zote lazima ziondolewe,” alisema

Alisema takwimu zinaonyesha utekelezaji wa mpango kipindi cha kwanza umechangia kupungua umasikini kwa mahitaji ya msingi kwa kaya kwa asilimia 10 na umasikini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12 kwa kaya masikini nchini.

“Wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili, Rais John Magufuli aliagiza kabla ya shughuli zozote za kipindi cha pili kuanza uhakiki wa walengwa ufanyike kote nchini ili kuondoa kaya zote za walengwa ambao zimepoteza sifa,” alisema

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halimashauri ya wilaya ya Iringa, Robert Masunya alisema mafunzo yaliyofanyika yamelenga kujenga uelewa wa pamoja na namna zoezi hilo la uhakiki litakavyofanyika.

“Uelewa na weledi katika zoezi hili utaondoa taharuki na sintofahamu kwa walengwa hivyo watendaji wote wanatakiwa kuwa wasikivu na kufatilia mafunzo ili kutoruhusu kurudia makosa,” alisema Masunya.

Masunya alisema, mkazo mkubwa katika kipindi cha pili utawekwa katika kuwezesha kaya zitakazo andikishwa kwenye mpango kufanya kazi ili kuongeza kipato.

Aidha, kipindi hiki cha pili kitahakikisha huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendeleza rasilimali watoto ususani katika upatikanaji wa elimu na afya.

Naye, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Samweli Marwa alisema wapo baadhi ya walengwa walikuwa wakilalamika kujiunga na huduma za afya CHF lakini hawapati huduma walizotarajia.

Marwa aliwataka walengwa wa Tasaf katika kipindi hiki cha awamu ya pili kujiunga katika huduma za aya kwani wanatarajia kufanya maboresho katika eneo la afya ili kuwasaidia kumudu gharama za matibabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!