Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Michezo Malinzi, Mwesigwa wana kesi ya kujibu – Mahakama
Michezo

Malinzi, Mwesigwa wana kesi ya kujibu – Mahakama

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ambaye amekuwa akikabiliwa na mashitaka 30 likiwemo la kutakatisha fedha. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Uamuzi huo pia umemkuta Selestine Mwesigwa ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo wakati wa uongozi wa Malinzi. Kabla ya kuingia TFF, Mwesigwa aliwahi kushika wadhifa wa ukatibu mkuu kwenye klabu ya Yanga yenye makao makuu yake kwenye makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga, Dar es Salaam.

Kutokana na uamuzi huo uliotolewa leo na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde, sasa wanamichezo hao, pamoja na wenzao wawili wanapaswa kujiandaa na utetezi katika hatua ya kuishawishi mahakama itengue uamuzi wake huo wa kuwakuta na kesi ya kujibu.

Wakati Malinzi na Mwesigwa wakikutwa na kesi ya kujibu na kutarajiwa kujitetea mbele ya mahakama hiyo, Meneja Ofisi wa TFF, Miriam Zayumba, ambaye ni mtuhumiwa wa nne, ameachiwa huru baada ya mahakama kujiridhisha kuwa hakuguswa na ushahidi wowote kati ya uliowasilishwa na upande wa mashitaka kupitia mashahidi 15 na vielelezo tisa.

Uamuzi wa kukutwa na kesi ya kujibu katika kesi hiyo Na. 213 ya mwaka 2017, unawahusu pia aliyekuwa mhasibu TFF, Nsiande Mwanga na Flora Lauya, aliyekuwa karani katika shirikisho la soka nchini.

Usikilizaji wa ushahidi ulianza Mei mwaka jana 2018 mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri ambaye baadaye alilazimika kuachana na kesi baada ya kupandishwa cheo alipoteuliwa kuwa jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kesi hiyo imekuwa ikiendeshwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (PCCB) na Mwanasheria Leonard Swai aliongoza mashahidi hao kutoa ushahidi kuhusiana na mashitaka ya udanganyifu, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi nyaraka, kula rushwa na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma uamuzi mbele ya wasikilizaji waliojaza chumba cha mahakama, Hakimu Mkazi Kasonde amesema kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, Malinzi, mshitakiwa wa kwanza, ameguswa na shitaka la tano la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, shitaka la 27 na la 28 linalohusu utakatishaji wa fedha.

Anatuhumiwa kutakatisha fedha ambazo ni Dola 173,335 na Sh. milioni 43.1 wakati Mwesigwa anakabiliwa na mashtaka sita ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutakatisha fedha.

Shauri hilo litaendelea kusikilizwa tarehe 6 Agosti mwaka huu ambapo washtakiwa wataanza kujitetea juu ya mashtaka yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!