August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Malinzi ateuliwa kuwa Mjumbe wa FIFA

Jamal Malinzi, Rais wa TFF

Spread the love

JAMAL Malinzi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka katika kipindi cha miaka minne.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa TFF, iliyosainiwa na katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samoura, ilisema uteuzi huo unaanza mwaka huu 2017 mpaka 2021 huku majukumu ya kamati hiyo ni kusimamia mipango ya mpira wa miguu duniani kote.

Kamati hiyo ambayo itaongozwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Asia itakuwa na wajumbe wengine kutoka nchi wanachama wa FIFA ambao watatangazwa kupitia mtandao wa shirikisho hilo.

Huu utakuwa mfululuzo kwa Malinzi kuteuliwa katika kamati tofauti za mashirikisho ya kimataifa ya mipra wa miguu, mwaka jana shirikisho la soka barani Afrika CAF lilimteua Malinzi kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati maalumu iliyoongozwa na Rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou.

error: Content is protected !!