April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Malinzi ahukumiwa  jela au faini

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam imemuhukumu Jamali Malinzi aliyekuwa Rais  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa aliyekuwa Katibu wa shirikisho hilo, kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Uamuzi wa kesi hiyo namba 213 ya mwaka 2017, ulioandaliwa na Hakimu Mkazi Maira Kasonde ambaye kwa sasa amehamishwa katika mahakama hiyo umetolewa leo tarehe 11 Desemba 2019, ambapo mshtakiwa Malinzi amekutwa na hatia ya kughushi nyaraka za uongo ili kujipatia fedha amehukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh.500000.

Mwesigwa alitiwa hatiani kwa kutumia nyaraka hizo amehukumiwa kwenda jela au kulipa faini kiasi cha Sh.1 Milioni.

Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Frola Rauya ambaye alikuwa karani.

Washtakiwa Malinzi na Mwesigwa wamekubali kulipa faini.

Washtakiwa hao walishtakiwa kwa makosa 20 yakiwemo kughushi nyaraka za uongo,nakujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha ambazo ni Dola 173,335 za Marekani.

error: Content is protected !!