Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Malima aachiwa huru
Habari Mchanganyiko

Malima aachiwa huru

Adam Malima (katikati) akitoka mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana
Spread the love

MAHAKAMA ya Mkazi Kisutu imemuachia huru Naibu Waziri wa Fedha wa awamu ya nne, Adam Malima leo kwa dhamana ya shilingi milioni tano, anaandika Hamisi Mguta.

Mapema leo Malima alifikishwa katika mahakama hiyo akituhumiwa kuwazuia polisi kufanya kazi yao.

Mlalamikaji katika kesi hiyo ni askari H.7818 PC Abdul akiwa kazini na maafisa wa Kampuni ya PBEL inayojihusisha na kukamata watu wanaopaki magari sehemu zisizotakiwa ambapo tukio hilo lilitokea jana eneo la Double Tree Hotel Masaki.

Mlalamikaji amedai alizuiliwa kutekeleza wajibu wake na waziri mstaafu huyo huku akishirikiana na wanachi kuwazuia askari hao ambapo askari huyo aliamua kupiga risasi sita hewani ili kuwatuliza watu waliokuwa wanazomea wakiongozwa na mtuhumiwa.

Hata hivyo mtuhumiwa pamoja na dereva wake walikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Oysterbay jana na kufunguliwa kesi yenye namba OB/RB/7306/2017.

Awali akizungumzia tukio lililotokea hadi kupelekea kesi Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema ni sahihi kisheria Malima kuchukuliwa hatua kwani kuzuia gari isikamatwe ni kuzuia kazi ya askari.

Hata hivyo Kamishna Sirro amesema kwakuwa katika eneo la tukio kulikuwa na mzozo na mabishano kati ya watu wa pembeni, Malima na Jeshi la Polisi ilimlazimu mmoja wa askari kupiga risasi tatu hewani kitendo ambacho amekitafsiri kama ni maamuzi ya busara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

error: Content is protected !!