Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maleko awataka wanawake kupaza sauti ulawiti watoto wa kiume
Habari Mchanganyiko

Maleko awataka wanawake kupaza sauti ulawiti watoto wa kiume

Spread the love

 

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Kilimanjaro, Esther Maleko, amewataka wanawake nchini kupaza sauti katika kupinga vitendo vya kikatili na ulawiti kwa watoto wa kiume, vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu katika maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanga … (endelea).

Maleko ameyasema hayo hivi karibuni alipotembelea vikundi vya akina mama wa UWT vinavyojihusisha na shughuli za ujasiriamali.

Amesema Serikali imeweka kipaumbele katika kuhakikisha inawezesha wanawake kiuchumi ili waweze kujikwamua na kuondokana na umaskini.

Amesema kuwa mwanamke wakiwezeshwa kiuchumi hata vitendo hivyo vya ukatili vitapungua kutokana na kwamba watakuwa karibu na watoto wao.

“Wamama msikubali hakikisheni tunaungana kwa pamoja kuupinga ukatili huu ambao wanafanyiwa watoto wetu wa kiume huko majumbani na baadhi ya wazazi na shuleni hili siyo jambo la kulifumbia macho, tuwe na kauli moja tusema sasa basi yatosha,” amesema Maleko.

Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Kilimanjaro, Esther Maleko

Amesema kuwa tatizo hilo likiachwa likaendelea litaathiri nguvu kazi ya Taifa na kukosekana viongozi bora wa baadae.

Katika ziara yake Maleko alikutana na kikundi cha wakina mama Maghariba waliokuwa wakijihusisha vitendo vya ukeketaji ambapo kwa sasa wameachana na shughuli hizo baada kupatiwa elimu na kufunguliwa mradi wa utengenezaji wa majiko banifu ili kujipatia kipato.

Nao baadhi ya Mangariba hao wamesema wameachana na shughuli za ukeketaji baada ya kuelemishwa kuhusu madhara ya ukeketaji na kuwezeshwa kiuchumi kwani walikuwa wakitumia shughuli hizo kujipatia kipato cha kuhudumia familia zao ambapo kwa siku walikuwa wakipata 20000 hadi 30000.

Sauda Msangi amesema kuwa kwasasa wameachana na shughuli za ukeketaji na kwamba wamejikita katika shughuli za ujasiriamali na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.

Katika ziara yake Maleko ametembelea kikundi cha wanawake cha Jikomboe kinachojihusisha na shughuli za fyatua matofali kilichopo Mgagao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!