May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Malawi kuwasili kesho, kujipima na Taifa Stars

Spread the love

 

Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinategemea kuwasili jijini Dar es Salaam kesho, kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu, dhidi ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) utakaopigwa jumapili tarehe 13 Juni, 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo utachezwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA), kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Msafara wa kikosi hiko cha Malawi utakuwa na watu 33, ambapo utawasili majira ya saa 2 usiku, kwa Shirika la ndege la Ethiopia.

Tayari kikosi cha Taifa Stars chini ya Kim Poulsen tayari kipo kambani kwa ajili ya mchezo huo, ambapo kiingilio cha chini kitakuwa shilingi 2,000.

Kiingilio kingine kitakuwa shilingi 5,000 kwa VIP B na C.

error: Content is protected !!