September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Makurumla waomba punguzo la riba, rejesho la mkopo

Spread the love

WANANCHI wa Kata ya Makurumla katika Jimbo la Ubungo, wamemuomba Rajabu Hassani, diwani wa kata hiyo kuwafikishia maombo yao ya punguzo la riba na marejesho kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, anaandika William Hezron.

Maombi hayo yametolewa leo katika mkutano uliowakutanisha Azizi Himbuka, Katibu wa Jimbo la Ubungo, diwani huyo na wafanyakazi wa Benki ya Biashara (DCB) waliopewa jukumu na manispaa kusimamia utoaji wa mikopo hiyo.

Mwananchi Asha Ally alitoa wito wa kumuomba diwani huyo kuzungumza na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jackob kuhusu kuangalia namna ya kupunguza riba na rejesho la wiki kutoka 20,000 hadi kufikia 10,000.

“Diwani naamini unajua hali zetu watu wa Makurumla ni ngumu hivyo kulipa marejesho ya 20,000 kwa wiki, hatutaweza ila tunaomba ukazungumze na Meya ili akarekebishe mkataba na Benki ya DCB na turudishie marejesho yapunguzwe sambamba na riba,” anasema.

Baada ya maombi hayo Hassani amewaahidi kuongozana na wawakilishi 10 walioteuliwa kwenye mkutano huo kwenda nao kwa Meya kuwasilisha kilio hicho.

error: Content is protected !!