May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makosa makubwa ya uhalifu yaongezeka nchini

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amesema jumla ya makosa makubwa 39,182 yameripotiwa katika vituo vya polisi katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Masauni ameyasema hayo leo Alhamisi tarehe 5 Mei, 2022 Bungeni jijini Dodoma akiwasilisha makadirio ya bajeti yam waka 2022/23.

Waziri huyo amesema idadi hiyo ni sawa na ongezeko la makosa 1,932 sawa na asilimia 5.2 ikilinaganiwa na makosa 37,250 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2020/2021.

“Kati ya makosa yaliyoripotiwa, upelelezi wa kesi 15,339 ulikamilika na watuhumiwa 16,514 walifikishwa mahakamani,” amesema Masauni.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni

Amesema kati ya kesi hizo 2,673 zilishinda, kesi 388 zilishindwa na kesi 12,278 zinaendelea kusikilizwa mahakamani.

“Katika mwaka 2022/2023 Jeshi la Polisi litahakikisha kuwa kesi zote zinapelelezwa kwa haraka ili wahusika waweze kufikishwa mahakamani.

Aidha, amesema jeshi hilo litaendelea kuboresha utendaji kazi wa maafisa, wakaguzi na askari kwa kutoa mafunzo na kutumia vifaa vya kisasa pamoja na kusimamia nidhamu na uwajibikaji ndani ya Jeshi la Polisi.

Masauni alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wananchi kutii sheria bila shuruti na kuzingatia maadili ya jamii.

error: Content is protected !!