October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Makontena ya vifaa vya walemavu hatarini kuuzwa

Spread the love

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya (Unity in Diversity Foundation) inayojishugulisha na huduma za kijamii za kugawa misaada ya walemavu imeiomba serikali kuondoa kodi kwenye bidhaa hizo. Anaandika Michael Sarungi … (endelea).

Akizungumza na waadishi wa habari mratibu wa taasisi hiyo taifa Enock Bigaye alisema kama taasisi wanaiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa mapana na kutoa msamaha wa kodi.

“Kama taasisi toka tuanze huduma hii tumeshaiingiza zaidi ya makontena 20 na kuyagawa bure kupitia kwa wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya, wizara na wakati mwingine wabunge” alisema Bigaye

Amesema kama taasisi wanatoa ombi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli aliangalie suala hili kwa mapana ili tuweze kusamehewa kodi kwenye bidhaa hizi zinapofika bandarini.

Amesema taasisi yake mpaka sasa kwa kushirikiana na taasisi ya (Universal Ministry of Africa) wamefanikiwa kuagiza na kiungiza nchini kontena mbili za vifaa vya msaada ambapo moja ni la vitabu vya piece elfu 25 ndani lenye thamani ya zaidi ya milioni 190.

Amesema kuna kontena la vifaa vya ufundi stadi ambapo ndani kuna computer laptop, vyarahani, mechanical equipment, carpentry hivyo vyote vimekwama.

“Mpaka sasa tunapozungumza nanyi (notification letter) vifaa vinataka kuuzwa mpaka sasa vipo ticks” amesema Bigaye.

Amesema hata hivyo pamoja na jitihada zote hizo mpaka sasa wana kuwa mali hiyo ipombioni kuuzwa kwa kudaiwa kodi.

Amesema walisha mwandikia rais barua tatu hatujui kama zilishamfikia, pia katibu mkuu kiongozi (Ikulu), katibu mkuu tamisemi hata hivyo mpaka sasa hatujapata mrejesho.

Amesema kitendo cha wao kupokea misaada toka kwa wahisani na kuizuia kwa ajili ya kodi ni sawa na kuwakosesha fursa watoto wetu pamoja na ndugu zetu walemavu ambao wangenifaika na misaada hii.

Amesema ni jukumu letu kuwajali watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha wanapata elimu kama watu wengine kwa kuondoa vikwazo vilivyoko mbele yetu.

error: Content is protected !!