July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makongoro: Mafisadi wanapora CCM

Mtangaza nia wa kuwania Urasi wa CCM, Charles Makongoro Nyerere

Spread the love

UPO uwezekano kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuporwa na mafisadi, vibaka na wezi iwapo hakitakuwa makini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Makongoro ambaye ni mtoto wa mwasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere pia amesema, ndani ya CCM kuna vibaka, wezi na mafisadi ambao wanajulikana na wao wanajijua.  

Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejesha fomu yake ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwa ngari ya urais.

Mgombea huyo ambaye alikuwa wa pili kurejesha fomu amesema, kuna wasiwasi mkubwa wa CCM kuwekwa mifukoni na mafisadi, vibaka na majambazi ndani ya chama.

Na kuwa, CCM inawajua vizuri mafisadi kama hawatakemewa ni wazi kuwa chama kitawekwa mfukoni na watu wachache.

“CCM ni chama cha watu wote, wakulima na wafugaji na wafanyakazi na kama viongozi ndani ya CCM hawatakuwa makini kuwadhibiti, ni wazi kuwa mafisadi hao watakiteka chama na kuwaweka wengine mifukoni.

“Kitakachofuatia hapo ni kukupora chama hicho na kubadilisha katiba na hapo ndipo wataanza kuitana, vibaka, wezi na mafisadi jambo ambalo litakuwa gumu tena kukirejesha chama hicho ambacho kwa sasa kinaaminika,” amasema Makongoro.

Amesema, kuna kila sababu ya viongozi ndani ya chama kutenda haki kwa wanachama wote au wagombea wote kutokana na kuwepo kwa dalili za watu kuvuja taratibu na kanuni ndani ya chama.

“Tulipopewa fomu tulitakiwa kila mgombea kutafuta wadhamini 30 kila mkoa lakini kuna watu ambao wamevunja masharti hayo na wengine wanatafuta wadhamini kana kwamba wanafanya kampeni sasa watu hao wanatakiwa kuangaliwa kwa makini zaidi ili haki itendeke kwa wote,” amesema Makongoro.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe akichukua fomu amesema kuwa, amelazimika kuchukua fomu kutokana na kuwa anatosha kuongoza nchi.

Akizungumzia vita yake na tuhuma mbalimbali ambazo ziliwapata baadhi ya wana-CCM wenzake aliposoma ripoti ya Richimond alisema kuwa, yeye hana adui yoyote hivyo hataki kuchafuliwa wala kumchafua mtu mwingine.

Hata hivyo alisisitiza kuwa, kilichowasilishwa katika ripoti hiyo ndicho sahihi na wala hakuna mtu ambaye anaweza kupindisha.

error: Content is protected !!