Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makongoro ataka ‘macho’ Mirerani, Biteko amjibu
Habari Mchanganyiko

Makongoro ataka ‘macho’ Mirerani, Biteko amjibu

Waziri wa Madini, Dotto Biteko
Spread the love

MKUU wa mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere ameitaka Serikali kurejesha watu maalumu wa kufuatilia mienendo ya mauzo ya madini ya Tanzanite maarufu kama ‘macho’ katika mji huo wa Mirerani ili kudhibiti utoroshaji na ukwepaji kodi katika biashara hiyo adhimu nchini. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo …. (endelea).

Pia amewataka maofisa madini mkoa wa Arusha na Dar es salaam kuhakikisha mnyororo wa biashara ya madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana eneo hilo la Mkoa wa Manyara, unarejeshwa na kufanyika ndani ya mkoa huo kwa kufuata maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kunufaisha mkoa huo kama yalivyo maeneo mengine ya machimbo ya madini dhahabu na almasi.

Makongoro ametoa wito huo leo tarehe 27 Agosti, 2022 mjini Mirerani mkoani Manyara katika hafla ya kumtangaza mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite, Anselim Kavishe kuwa bilionea mpya baada ya kupata vipande viwili vya madini hayo vyenye thamani ya Sh bilioni 2.2.

Amesema ‘macho’ hao walikuwa na faida kwa kuwa walikuwa wanaangalia kwa niaba ya serikali lakini sasa halali kwa amani kwani hajui nini kinachoendelea katika eneo hilo.

Aidha, amesema katika maeneo ya Kahama kuna huduma muhimu kama vile za maji, barabara kutokana na uchimbaji wa madini ya almasi ambayo yanapatikana sehemu mbalimbali duniani lakini inashangaza kuona Mirerani huduma hizo hakuna ilihali ndipo panapochimbwa madini pekee ya Tanzanite.

“Nahisi kuna mtu ananishika jezi sehemu fulani. Nikiangalia nahisi kuna mtu ananifanyia mambo kihuni. Wote tuna kupata shangwe mabilionea lakini kuna mtu ananishika jezi, tushirikiane nikimbaini anayefanyia mambo ya kihuni tushughuli naye,” amesema.

Aidha, akizungumzia hoja hizo, Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema mfumo wa awali wa kuweka macho katika eneo hilo la machimbo ulikuwa na udhibiti dhaifu kiasi cha watu hao waliowekwa kwa niaba ya serikali ‘kula dili’ na wachimbaji kisha kuikosesha serikali mapato.

Hata hivyo, amesema sasa kuna macho au watu nane ambao wanafanya kazi hiyo kwa siri kwa niaba ya serikali tofauti na awali ambapo walikuwepo sita wanaofahamika.

Kutokana na hali hiyo amesema sekta ipo salama chini ya Samia kwani wanaofanya kazi hiyo ni waajiriwa wa serikali waliotoka kwenye vyombo vya dola.

“Chini ya Samia mapato ya sekta ya madini yameongezeka kutoka Sh bilioni 475 hadi bilioni 623 katika kipindi kifupi.

Samia amekuta mchango wa sekta ya madini ukiwa asilimia 5.7 mwaka huu 7.9,” amesema.

Kuhusu mnyororo wa kibiashara katika eneo hilo la Mirerani, Biteko amesema kukamilika kwa mji wa Tanzanite ndiko kutauwezesha mji huo kunufaika vema na madini hayo.

“Ni kweli maeneo mengine yameendelea vizuri kwa sababu ya migodi ya Buzwagi, Bulyanhulu huko Kahama na Geita inatoa fedha za kutosha za uwajibika kwa kampuni kwa jamii.

“Mathalani Kahama wanapata Sh bilioni tano kwa mwaka wakati Geita wanapata Sh bilioni 10, hivyo kwa Mirerani ni lazima tufanye kazi kubwa kwa wachimbaji kuchangia maendeleo ya jamii,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

error: Content is protected !!