February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Makonda: Mashoga wamekimbia Dar, wamehamia Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuna baadhi ya watu wanaofanya biashara ya kuuza mwili (machangudoa na mashoga) wamehamia Dodoma ili kutafuta soko. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 31Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam.

Amesema, tangu serikali itangaze Dodoma kuwa makao makuu ya nchi, kuna watu walishaanza kutangulia mkoani humo, ambapo wengi wao wanatoka jijini Dar es Salaam.

“Na kama mnakumbuka pale waliposema makao makuu ya nchi yanakuwa Dodoma kuna watu walishaanza kutangulia Dodoma kama sehemu ya kujua soko lao linapatikana kule, na hao wanaofanya hivyo wanatoka Dar es Salaam,” amesema na kuongeza.

“Kuna watu wametoka Buguruni wameanzisha madanguro yao Bagamoyo, Mpanda Arusha  na Dodoma.Sio jambo jema.”

error: Content is protected !!