KUFUATIA mvua zinazoendelea kunyesha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa mkoa wake kuwa na tahadhari ili kuhepuka mafuriko. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).
Makonda ametoa kauli hiyo leo tarehe 9 Oktoba 2019, wakati akizindua mfumo wa kupokea kero za wananchi na malalamiko dhidi ya watendaji.
“Tunazidi kuwasihi sana wananchi kujenga kwa kufuata mipango miji, lakini pamoja na jitihada ambazo serikali imeendelea nazo naomba niwasihi wananchi kuona umuhimu wa kufanya usafi,” amesema.
Amesema, kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), mvua zitaendelea kunyesha zaidi na kwa sababu mji huo upo chini kutoka usawa wa bahari, wananchi wanapaswa kuwa makini hasa wanaoishi mabondeni.
“Nawapa pole wanaopata changamoto na ni vyema tukaendelea kujihadhali na kuchukua hatua mapema iwezekanavyo,” amesema.
https://youtu.be/PjpsO_T1OK4
Katika hatua nyingine Makonda amezindua mfumo maalum wa kufikisha malalamiko kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia namba ambazo kila wilaya imepewa.
“Kutuma ujumbe huu ni bure ambapo unatuma ujumbe kwa kuanza na neni DSM na kuandika ujumbe wako kisha unatuma kwenda namba 11000 au kwa wanaotumia mtandao wanaweza kutuma malalamiko yao kupitua www.malalamiko.dsm.go.tz,” amesema.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge amesema kuwa kadri ambavyo mfumo huo utaendelea kutunika, unakubali kuongeza mahitaji mengine kadri yatakavyohitajika kulingana na wakati husika.
Leave a comment