May 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Makonda kujitosa ubunge, mjadala waibuka

Paul Makonda, Mtia nia jimbo la Kigamboni

Spread the love

HATUA ya Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kugombea ubunge katika Jimbo la Kigamboni, imeibua maswali. Anaandika Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Makonda amechukua fomu hiyo leo tarehe 15 Julai 2020, jijini Dar es Salaam huku hoja kubwa iliyoibuka kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu kama amejiuzulu ama la.

Tayari Rais John Magufuli alitoa onyo kwa wateule wake wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali kwenye ngazi mbalimbali, nafasi zao hazitawasubiri.

Rais Magufuli alisema, mteule wake atakayeomba ruksa kwenda kugombea atampatia na nafasi yake itajazwa pasina kusubiri kurejea baada ya mchakato wa kupata wagombea kukamilika.

Mjadala kwenye mitandao ya kijamii hususani twitter, umejielekeza kuhusu kujiuzulu kwake lakini pia nafasi ya Dk. Faustine Ndungulile, aliyekuwa Naibu Wazir wa Afya, ambaye ndiye mbunge anayemaliza muda wake kwenye jimbo hilo.

Soma zaidi hapa

Uchaguzi Mkuu 2020: JPM ‘Ukiniomba ruhusa nakupa lakini…’

Mtu anayejitambulisha kwa jina la @JengelaChriss, ameandika “kwa hiyo amepumzika ukuu wa mkoa au bado anaendelea na nafasi yake ya ukuu wa mkoa huku akisubiri kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge?”

Jonahbmz kwenye ukurasa wake wa twitter ameandika, “mzee baba si alisema wajiuzulu kwanza? au nilisikia vibaya?” ameuliza.

Timothy96830693 amehoji kwamba, kwanini wakuu wa mikoa nao wanakimbilia ubunge na kwamba, Dodoma kuna nini?

“Sasa mbona kila mtu analimbilia Dodoma, kuna nini? Kwa nia njema au maslahi binafsi? Maana sasa Ukuu wa Mkoa mpaka Ubunge.”

FredOyoo9 amehoji “Duh! Kwa hyo kero za wanaKigamboni atazipelekea mkuu wa mkoa wa Dar?”

@abubadohu ameuliza “Mkuu wa Mkoa ameachia ngazi ya cheo chake au mpaka apitishwe?”

error: Content is protected !!