Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Makonda ‘aubeep’ mtandao wa ‘wauza unga’
Habari MchanganyikoTangulizi

Makonda ‘aubeep’ mtandao wa ‘wauza unga’

Spread the love

PAUL Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameutaja mtandao wa wauzaji wa dawa za kulevya hapa jijini huku miongoni mwao, yakiwemo majina ya wasanii maarufu pamoja na wafanyabiashara mbalimbali, anaandika Charles William.

Katika mkutano wake na wanahabari hii leo jijini Dar, Makonda amesema yupo tayari kupoteza kila kitu, ikiwemo maisha yake na ukuu wa Mkoa lakini awe na majibu kwa Mungu kuhusu mchango wake katika kukabiliana na uharibifu unaosababishwa na dawa za kulevya.

Wasanii Wema Sepetu, TID, Rachel, Chid Benz, Mr. Blue, Dogo Hamidu na Babuu wa Kitaa, mtangazaji wa kituo cha Clouds TV wametajwa kuwa na mahusiano na mtandao wa dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati kesho asubuhi kwaajili ya mahojiano zaidi.

Christopher Fuime aliyewahi kuwa Mkuu wa Polisi Mkoa Maalum wa Kipolisi Kinondoni (RPC) ni miongoni mwa maofisa 17 wa Jeshi la Polisi waliotajwa kushirikiana kuulinda mtandao wa dawa za kulevya jijini Dar.

“Polisi wamekuwa wakiwapigia simu watuhumiwa wa uuzaji wa dawa za kulevya na kuwataarifu kuwa wanaenda kuwakamata na kisha kuwataka wawatumie fedha kwa njia ya simu. Polisi wanapoenda wanawakosa wahusika lakini wanakuwa wameshapokea fedha zao,” amesema Makonda.

Makonda amewataja watu ambao tayari wanashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na tuhuma za kuuza dawa za kulevya akiwemo Said Masudi Lina, Ahmed Ngahemela “Pettit Man”, Nassor Mohamed, Bakari Mohamed Khelef na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Omary.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!