August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda atibua, Polisi kwawaka moto

Ernest Mangu, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)

Spread the love

SIKU mbili baada ya Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutaja majina ya wasanii na askari wanaotuhumiwa kuhusika na utumiaji pia biashara ya dawa za kulevya, askari 12 wamesimamishwa kazi, anaandika Hamisi Mguta.

Ernest Mangu, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) leo amewasimamisha kazi askari hao kwa lengo la kupisha uchunguzi baada ya kutajwa kushirikiana na wauza dawa za kulevya.

Waliotajwa kusimamishwa kazi ni pamoja na PF 14473 SACP Christopher Fuime, PF 17041 INSP Jacob Hashimu Swai, D 3499 D/ SGT Steven Apelesi Ndasha, E 8431 D/SGT Mohamedi Juma Haima, E 5204 D/ SGT Steven John Shaga, E 5860 D/ CPL Dotto Steven Mwandambo, E. 1090 D/ CPL Tausen Lameck Mwambalangani.

Wengine ni E. 9652 D/CPL Benatus Simon Luhaza, D. 8278 D/CPL James Salala, E. 9503 D/CPL Noel Masheula Mwalukuta, WP 5103 D/C Gloria Mallya Massawe na F. 5885 D/C Fadhili Ndahani Mazengo.

Jana wasanii waliotajwa katika orodha ya wanaotuhumiwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ni Wema Sepetu, Babuu wa Kitaa, Khalid Mohamed (TID), Hamidu Chambuso (Nyandu tozi) walitii amri ya Makonda iliyowataka kufika kituo kikuu cha Polisi (Central) kwa mahojiano.

 

error: Content is protected !!