June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda athibitisha kipindupindu Kinondoni

Spread the love

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amethibitisha kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika wilaya hiyo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Makonda amethibitisha hayo leo ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari leo, huku akitoa tahadhari na kuwatoa hofu wakazi wa wilaya hiyo.

Makonda amesema kuwa ugonjwa huo uliibuka 15 Agosti, 2015 baada ya familia moja inayoishi Kijitonyama kwa Ali Maua kupata mgojwa huyo, uliosababisha mkazi mmoja kufariki huku familia hiyo ilifanya mazishi ya marehemu huyo bila tahadhari zozote.

Amesema kuwa kata zilizoathirika ni Kijitonyama, Kimara, Saranga, Manzese, Tandale, Makumbusho na Mwananyamala. Hospitali ya Mwananyamala imepokea wagonjwa 34 na Sinza imepokea wagonjwa 16 ambapo watatu wamefariki.

“Sisi kama serikali tumejipanga kukabiliana na ugonjwa huo, tuna dawa na vifaa tiba vya kutosha, pia tumefungua kambi yetu katika zahanati ya Kijitonyama,” anasema Makonda.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuzingatia kanuni za usafi ambazo ni kunawa mikono, kuchemsha maji, kula chakula cha moto na kuwahi hospitali mapema utakapoona dalili za ugonjwa huo.

Naye Daktari Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dkt Azizi Msuya amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo na kuwapa huduma ya kwanza wagonjwa kwa kuwapa maji yenye vuguvugu yaliyochanganywa sukari na kuwawahisha hospitali.

error: Content is protected !!