September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda amvimbia mteule wa JPM

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amefutilia mbali kauli ya Sofia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwamba ibada zifanywe siku maalum tu. Anaripoti Martin Kamote…(endelea).

Makonda ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari leo tarehe 22 Oktoba 2019, ofisini kwake huku akisisitiza ‘umakini kwa viongozi wa serikali kuzungumzia imani za dini.’

Tarehe 12 Oktoba2019, Mjema aliwaagiza maofisa kwenye wilaya yake kuhakikisha, ibada zinafanywa kwenye siku maalum (Ijumaa, Jumamosi na Jumapili) na si vinginevyo.

Akipingana na kauli hiyo, Makonda amesema, vingozi hawapaswi kuingilia siku za wananchi kuabudu na badala yake, wanapaswa kuwa makini wanapotaka kuzungumzia masuala ya imani.

“Viongozi tunapaswa kuwa makini tunapoingia kwenye mambo ya dini, mambo ya dini ni mambo ya imani, mimi mwenyewe hapa ni mlokole hunipangii muda wa kusali,” amesema Makonda na kuongeza “kwa kuwa mimi ndio mkuu wa mkoa huu, ibada nazitaka siku zote.”

Tazama video kamili hapo chini

error: Content is protected !!