July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda ahimiza wananchi kujiajiri

Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amewashauri Watanzania kuiga mfano kwa wawekezaji ili kujikwamua na umasikini badala ya kuilalamikia Serikali kwamba haitoi fursa za ajira. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Makonda ametoa rai hiyo jijini Dar es Salaam leo, wakati akizindua maonyesho ya Tanzania Home Expo, yaliyoandaliwa na EAG GROUP, yanayolenga kuwakutanisha wananchi na makampuni mbalimbali.

Maonyesho hayo yaliyoanza Mei 29 na yatamalizika 31 mwaka huu, yanashirikisha makampuni zaidi ya 62, ambayo yameweka mabanda yao katika ukumbi wa Mlimani City.

Amesema “nimejifunza vitu vingi sana katika mizunguko yangu, lakini hapa pamezidi kweli. Tunatakiwa kujifunza. EAG mmefanya vizuri kuleta haya maonyesho”.

Kwa mujibu wa Makonda, kuna umuhimu wa Watanzania hususani vijana kujifunza na kupanua mawazo yao jinsi ya kuweza kujipatia ajira.

Pia, amewashauri wajifunze kutoka kwa vijana wenzao ambao wameelimika, wawekezaji nchini na kutumia fursa zilizopo.

“Sio kwamba Tanzania ina uhaba wa ajira kama inavyodaiwa, ajira zipo nyingi sana, tuitumie ardhi yetu kujiajiri hata ukiwa mkulima ni ajira tosha,” amesema Makonda.

Ameongeza “tuwaepuke sana wanasiasa ambao wanawapoteza na kuwaambia kwamba fursa za ajira hakuna, ni waongo wakubwa hawana cha kusema pindi wakiwa jukwaani,”amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya EAG Group, Imani Kajula, amelieleza MwanaHALISIOnline kuwa, mwitikio wa watu katika maonyesho hayo ni mkubwa, tofauti na ya mwaka jana.

Amesema, “kitu kingine kinachoonyesha kuwa Watanzania na makapuni mengi yanakubali maonyesho hayo ni pale mbapo makampuni yameendelea kushiriki nasi”.                                                                                                                           

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu juu ya mambo mengi ambayo yamekuwa yakileta utata pindi wanapohitaji misaada mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi na mikopo.

error: Content is protected !!