January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda aburuzwa mahakamani, kesi Desemba 3

Paul Makonda

Spread the love

 

HATIMAYE Paulo Christian Makonda,  ameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kujibu mashitaka ya jinai yanayomkabili.  Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwanasiasa huyo aliyetikisa katika utawala wa awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, ametuhumiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds cha Dar es Salaam, Machi mwaka 2017, matumizi mabaya ya madaraka na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Kesi dhihi ya Makonda, aliyepata kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, imepangwa kutajwa tarehe 3 Desemba 2021 na tayari Mahakama imetoa amri ya wito kumtaka kufika mahakamani siku hiyo.

Anadaiwa kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds, 2017, kuingilia maudhui ya matangazo ya Clouds, kuvamia ofisi za kituo hicho akiwa ameongozana na maafisa wa majeshi, mambo ambayo ni kinyume cha sheria za nchi.

Habari zaidi soma Gazeti la Raia Mwema la leo Jumamosi, tarehe 27 Novemba 2021.

error: Content is protected !!