July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makonda aanza kwa tambo

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akikagua miradi ya wilaya hiyo

Spread the love

MKUU wa Wilaya wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Paul Makonda, ameainisha kero nne atakazoanza kuzipatia ufumbuzi. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea)

Kero hizo ni afya, elimu, ardhi na maji ili kupunguza usumbufu kwa wananchi na kuwaondolea umaskini.

Makonda ametoa ahadi hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake, baada ya ziara fupi ya kukagua shule ya Sekondari Tuliani na Manzese zilizopo ili kuangalia ujenzi wa maabara unavyoendelea.

Kwa mujibu wa Makonda, atatekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la kukamilisha ujenzi wa maabara hizo kabla ya Juni mwaka huu.

“Nitahakikisha wananchi wangu katika kata zote za Kinondoni wanapata elimu bora, kutoka kwa waalimu bora na shule zote zikiwa na vifaa vyote.

“Leo nimeanza kutembelea hizi shule mbili na baadaye nyingine zitafuata ili nione changamoto zilizopo na jinsi ya kuzitatua,” amesema Makonda.

Hata hivyo, Makonda ameeleza kuwa, Kinondoni ni moja ya Wilaya inayoongoza kuwa na wakazi wengi kiasi kwamba changamoto ni nyingi ikiwemo migogoro ya ardhi, ambapo ameahidi kutatua tatizo hilo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wake.

“Nipo tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya wananchi wangu ili kuhakikisha kila mtu anapata haki yake. Kuna mpango ambao nitauanza kuanzia Machi 6, mwaka huu.

“Kila jumaa nitakuwa hapa ofisini kwangu kusikiliza wananchi wenye migogoro ya ardhi na nitakuwa natoa hukumu hapo kwa hapo… kama ulidhurumiwa basi utarejeshewa haki yako,” amesema Makonda.

Anasisitiza kuwa atakua sambamba na wananchi wake katika masuala ya kutetea haki zao, hususani ajira kwa vijana.

error: Content is protected !!