December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makinda: Matokeo ya sensa yataendelea kutolewa

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, Anna Makinda

Spread the love

 

KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, Anna Makinda, amesema matokeo ya zoezi hilo yataendelea kutolewa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza matokeo ya mwanzo, leo Jumatatu, tarehe 31 Oktoba 2022. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mama Makinda ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, katika uzinduzi wa matokeo ya zoezi hilo lililofanyika tarehe 23 Agosti 2022.

“Leo tupo hapa kuanza awamu ya tatu ya kutangaza, haya ni matokeo ya mwanzo ya sensa kama mlivyoona katika dodoso kuu ya sensa tulivyokuwa tunahesabiwa kulikuwa na maswali zaidi ya 100 na matokeo atakayozindu Rais yanatokana na uchambuzi wa maswali machache kati ya hayo,” amesema Mama Makinda.

Mama Makinda amesema “kadiri uchambuzi utakapokamilika ndivyo matokeo zaidi yatakavyoendelea kutolewa kwa mujibu wa kalenda ya kuchapisha matokeo ya sensa. Kwa hiyo matokeo ya mwanzo na mengine watakavyozidi kuchambua yataendelea kutokea. Kuna mambo ya ustawi wa jamii, mazingira na hali halisi, yataendelea kutolewa.”

Kamisaa huyo wa sensa amesema kwa sasa zoezi hilo liko awamu ya tatu ambayo inahusisha usambazaji wa takwimu zake na matumizi ya matokeo ya sense.

“Awamu hii inafanywa tathmini na kupokea changamoto mbalimbali ambazo zilitokea wakati tunajiandaa kupiga sensa ya 2022. Hizi changamoto zinatakiwa ziangaliwe kwamba sensa ya 2032 zisijirudie,” amesema Mama Makinda.

Akizungumzia kuhusu zoezi hilo, Mama Makinda amesema limewaunganisha Watanzania ambao walikuwa na shauku ya kujua matokeo ya sensa ya watu na makazi.

“Hatukuweza kufikiria hata kidogo kuwa suala hili la sensa linaweza kuvuta hisia za watanzania na kuwaleta pamoja kiasi hiki. Katika kipindi chote cha utekelezaji majukumu yetu tulikutana na watanzania wa makundi mbalimbali na jamii, ikiwemo viongozi wa dini, siasa, mila, siasa, wanataaluma, wasanii na vijana,” amesema Mama Makinda.

error: Content is protected !!