
Spika wa Bunge la Muungano, Anne Makinda
KUTOKANA na wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),kupingwa upitishwaji wa miswada mitatu ya inayohusu mafuta na gesi, Spika Anne Makinda amelazimika kutoa ufafanuzi wa jambo lililotokea bungeni. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Makinda amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 33(2) ya Kanunizabunge Toleo la Aprili, 2013), Julai 02 na 03 , 2015 siku ya Alhamisi katika Orodha ya Shughuli za siku hiyo Miswada minne ya Sheria iliorodheshwa ili ifanyiwe kazi katika hatua mbalimbali .
Makinda alizitaja hatua hizo kuwa ni Muswada wa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi wa Mwaka 2016.
Amesema mswada huo ulikuwa uendelee kwa hatua ya Kamati ya Bunge Zima, kwa kuwa hatua hiyo haikukamilika siku ya Jumatano tarehe 1 Julai, 2015 amesema mswada mwingine ni ule wa Sheria ya Petroli wa Mwaka 2015.
Katika miswada hiyo Makinda aliutaja muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015 na muswada wa Sheria wa Mwaka 2015 ambamo amesema Miswada hiyo mitatu ilikuwa imepangwa kwa ajili ya Kusomwa Mara ya Pili na hatua zinazofuata.
Akiendelea kutoa ufafanuzi Makinda anasema baada ya Kipindi cha Maswali mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema) alisimama na kuomba Mwongozo wa Spika na kueleza kwamba kwanza, Orodha ya Shughuli imekiuka Kanuni ya 53(1) na (6), na 86(1)(5) na (6).
Makinda akinukuhu maneno ya Mnyika alisema “Miswada yote ambayo imewahi kuja hapa Bungeni, hoja ikishatolewa ni lazima kwamba hoja hiyo ijadiliwe, iamuliwe ndiyo ije hoja nyingine. Hapa maana yake tumeletewa Order Paper yenye hoja juu ya hoja, kwa vyovyote vile Order Paper haipaswi kukubalika inapaswa kuondolewa.”
“Pili, Mheshimiwa Mnyika alieleza kwamba kitendo cha kuileta Miswada hii mitatu Bungeni ni kukiuka msingi wa makubaliano yaliyokuwepo kwenye Semina iliyofanyika tarehe 30 Juni, 2015 ambapo Wabunge waliikataa Miswada hii isiletwe kwa hati ya dharura”alisema Makinda.
Amesema baada ya maelezo ya Mnyika alitoa Mwongozo na kueleza kwamba hakuna utaratibu uliokiukwa kwa kuwa Miswada iliyoorodheshwa katika Orodha ya Shughuli imezingatia utaratibu wa Kanuni alizozinukuu kwa maana kwamba kwanza Bunge litakamilisha hatua iliyobaki kwa Muswada ambao haukukamilika siku ya Jumatano na baadaye kuendelea na Miswada mitatu iliyokuwa inafuata.
Amesema kilichofutia ni baada ya hapo ni fujo kama ambavyo kila ilivyoonekana na kulazimika kusitisha Shughuli za Bunge.
Amesema uamuzi wa kuipanga Miswada hiyo kwa pamoja ni kutokana na kikao cha Kamati uongozi iliyokutana 29 juni.
Akitoa ufafanuzi Makinda alisema 2 Julai, mwaka huu Kamati ya Uongozi katika Kikao chake cha tarehe 29 Juni, 2015.
Amesema katika vikao vya Kamati ya Uongozi vilivyotangulia, Wajumbe wote wa Kamati waliohudhuria waliridhika na maelezo ya Serikali juu ya umuhimu wa kuleta Miswada hii kwa Hati ya Dharura.
Amesema 26 Juni, 2015 kwa mujibu wa Kanuni ya 85(1) Makinda alipokea taarifa kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Murtaza Mangungu, alimtaarifu Spika kwa kumweleza kwamba Kamati imemaliza kazi yake.
Amesema kazi hiyo ilikuwa ni kuchambua na kuijadili Miswada husika na kwamba Kamati iko tayari kuwasilisha Bungeni Maoni na Ushauri wake.
Makinda amesema baada ya hiyo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Spika aliagiza Miswada hiyo iwekwe kwenye Orodha ya Shughuli kama Kanuni ya 85(2) inavyoelekeza.
Amesema jana Julai 3, 2015 baada ya kuupitisha Muswada wa Kuwalinda Watoa Taarifa ya Uhalifu na Mashahidi wa Mwaka 2015.
Spika amesema baada ya hatua hizo alimwita Katibu asome shughuli iliyofuata kwenye Orodha ya Shughuli za bunge.
“Katibu akasoma jina la Muswada, nami nikamwita Mtoa Hoja, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene awasilishe Muswada husika.
“Wakati Waziri Mtoa Hoja ameshaanza kusoma maelezo yake, Wabunge upande wa Upinzani walinyanyuka wengi na kuomba Mwongozo bila utaratibu. Waliendelea kufanya fujo hadi ikalazimu Shughuli za Bunge zisitishwe tena siku ya pili.
“Pamoja na uvumilivu ambao Kiti kimekuwa kikionyesha muda wote, sasa ilionekana dhahiri kuwa lengo la baadhi ya Wabunge wa Upinzani ni kuhakikisha kazi za Bunge hazifanyiki. Hivyo ilinilazimu kutumia Kanuni ya 74 ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili hatua zichukuliwe kwa wale walioonekana ni vinara wa utovu wa nidhamu”amesema Makinda.
Amesema kama wabunge walikuwa hawaitaki hiyo miswada ya Petrol na Gesi iwasilishwe wangeweza kufanya yafuatayo.
Amesema mambo ambayo yalitakiwa kufanyika ni kuhakikisha kuwa Kamati iliyopewa jukumu la kuchambua Miswada hiyo inaikataa baada ya kujadiliana na Serikali kama ilivyokuwa kwenye Muswada wa Haki ya Kupata Habari.
Alitaja hatua nyingine kuwa baada ya mjadala kuanza Bungeni wangeweza kutoa hoja kuwa mjadala usiendelee hadi siku nyingine, ili Mbunge yeyote anayekusudia kuleta marekebisho kwa mujibu wa Kanuni 88(1)apate nafasi ya kufanya hivyo.
Makinda amesema Kanuni hiyo inasomeka na kuelezea kuwa “Mtoa hoja au Mbunge mwingine anayekusudia kuwasilisha mabadiliko katika Muswada unaojadiliwa, anaweza kumwomba Spika kwamba, hatua ya kuingia katika Kamati ya Bunge Zima iahirishwe hadi wakati atakaoutaja katika ombi lake na Spika atatoa uamuzi wake kadri atakavyoona inafaa”
Amesema kwa kutumia Kanuni ya 90, Waziri mwenye Muswada anaweza akauondoa wakati wowote kabla ya Bunge kuhojiwa kutoa uamuzi.
“Hizi ni hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa muda wowote bila kujali kwamba Muswada umekwishapita kwenye Kamati na Spika kutaarifiwa na Mwenyekiti wa Kamati kuwa Kamati yake imekamilisha kazi na umepangiwa muda wa kujadiliwa,”amesema
“Aidha, Miswada kuletwa kwa Hati ya Dharura ni utaratibu wa kawaida. Hatua nyingine zote hufuatwa isipokuwa katika Mkutano huo huo Muswada husoma Mara ya Kwanza na hatua zake zote” alieleza.
Amesema jambo hilo limefafanuliwa kwa kina kwenye Kanuni ya 80(4)-(6).
Amesema kanuni ya 80(5) imeeleza wazi kuwa Hati ya Dharura haiwezi kukubalika hadi Kamati ya Uongozi iikubali na iridhishwe na sababu za kuiwasilisha Miswada husika kwa Hati ya Dharura.
Amesema Miswada hayo yote yalifanyika kwa kufuata utaratibu na Spika alitimiza wajibu wake kupeleka Miswada hiyo kwenye Kamati ya Kudumu ili waifanyie kazi kwa maana ya kualika wadau na kushauriana na Serikali.
“Katika hatua hii Muswada ungeweza kukataliwa kwenye ngazi ya Kamati na Spika kuelezwa sababu,” amesema.
Amesema hoja kwamba wadau au Semina ilikataa Miswada hii isiwasilishwe Bungeni haina nguvu kwenye Kanuni za bunge.
“Kwa mujibu wa Kanuni ya 84(2) Kamati hupokea maoni ya watu wengi, baadaye Kamati ina wajibu wa kuangalia maoni hayo kama yamesaidia kuuboresha Muswada. Taarifa ya Kamati haifungwi na maoni ya Wadau au lobbyist.
“Kilichofanyika na wenzetu ni kusudio la kuvuruga taratibu za Bunge kwa makusudi na kwa lengo la kuleta fujo.
“Kama ambavyo nimeeleza, Kamati zote zina Wabunge wa aina zote. Kama kuna hoja Miswada inaweza kubadilishwa na hata kuondolewa, kwenye ngazi ya Kamati,” amesema Makinda.
More Stories
Bawacha yasitisha kongamano la siku ya wanawake duniani
Rais Mwinyi amwapisha mrithi wa Maalim Seif
Mrithi wa Maalim Seif aahidi haya