Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makinda aziangukia AZAKI kuhamasisha sensa 2022
Habari Mchanganyiko

Makinda aziangukia AZAKI kuhamasisha sensa 2022

Kamishna wa Sensa na Makazi ya Watu Tanzania, Anna Makinda
Spread the love

 

KAMISHINA wa Sensa na Makazi ya Watu nchini Anna Makinda ameziomba Asasi za kiraia kuwahamasisha watanzania kujitokeza kuhesabiwa wakati wa siku ya sensa inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka 2022. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu ametoa kauli hiyo jana tarehe 27 Oktoba, 2021 wakati akizungumza na viongozi na wadau waliohudhuria kongamano la AZAKI lililofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Amesema Azaki zina nafasi kubwa ya kuifikia jamii na watu wenye rika mbalimbali hivyo ni jambo jema kufanya uhamasishaji ili jamii ijitokeze kuhesabiwa.

Amesema sasa kunafanyika zoezi la sensa ya majaribio ili kuweka mazingira mazuri ya maandalizi ya sensa ya mwaka 2022.

Amesema kutokana na kanuni na taratibu za Umoja wa Mataifa, sensa ya majaribio hufanyika mwaka mmoja kabla ya sena kuu kufanyika ambapo wataalamu hutakiwa kuanza maandalizi ya sensa ya mwaka mwengine.

“Sisi hapa Tanzania baada ya kumalizika kwa Sensa mwaka 2012 wataalamu wetu walikaa na kuona ni namna gani Sensa ya mwaka 2022 itakavyokuwa,” amesema Makinda.

“Kabla ya mwaka mmoja waliteuwa mikoa 18 ya majaribio, vijiji na vitongoji kadhaa lengo likiwa nikutaka kuona kama sensa ya mwaka 2022 maandalizi yako vizuri au kuna vitu vinatakiwa kuongezwa,” amesema.

Makinda amesema viongozi hao wamekutana na kuleta mrejesho kama sensa ya majaribio ili kufahamu changamoto zilizojitokeza kwenye madodoso, matumizi ya vishikwambi mengine.

“Tukumbuke Rais Samia Suluhu Hassan alizindua mkakati wa elimu na uhamasishaji wa Sensa 2022 lengo alitutaka sisi wasaidizi wake tuende kuwaelimisha wananchi ili ifikapo siku hiyo kila mtu aandikishwe na kuhesabiwa sehemu yoyote alipo” amesema.

Kwa upande wake Mtakwimu Mwandamizi Makao Makuu Dodoma, David Mwaipopo amesema tangu Tanganyika ipate Uhuru zoezi la sensa ya watu na makazi ilifanyika mara tano na kuwa na matokeo tofauti tofauti.

Mwaipopo amesema kuwa sensa ya watu na makazi ya mara ya kwanza ilifanyika mwaka 1967 chini ya utawala wa Rais Julius Nyerere na kuonesha Tanzania ilikuwa na watu milioni 12 na ile ya mwaka 1978 na kulikuwa na watu milioni 17.

“Sensa ya nyingine ilifanyika mwaka 1988 chini ya utawala wa Rais Ali Hasan Mwinyi ambapo kulikuwa na watu milioni 23, mwaka 2002 chini ya utawala wa Rais Benjamini Mkapa watu walikuwa milioni 34 na mwaka 2012 chini ya Uongozi wa Jakaya Kikwete watu walikuwa milioni 44.5″amesema Mwaipopo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!