January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makinda amwogopa Magufuli

Spread the love

WAKATI akitafutwa Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wengi wamejitokeza kutaka kiti hiko huku Anne Makinda ambaye alidhaniwa kuwa jina lake litakuwa miongozi mwa mwao likiwa halipo kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni ‘kumwogopa Rais Magufuli’. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vimeonyesha kuwa huenda Makinda anaogopa kasi ya Rais mpya wa Jamhuri, Dk. Magufuli ambaye ameonekana akiweka mkazo katika utendaji kazi kwa watumishi wa Serikali.

Kutokana na Rais Magufuli kujionyesha kuwa ni mtu wa kazi na mwenye kupenda watendaji wachapakazi mara baada tu ya kuapishwa, huenda spika huyo ameona ni vyema kutulia kwakuwa Spika ajaye atakuwa na sifa ya ziada ya kumsoma rais na kwenda na kasi yake ili kuhakikisha nchi inasonga mbele.

Ingawa Makinda alisikika akitaja sababu zilizomfanya asichukue fomu ya uspika kwenye mkutano na waandishi wa habari jana katika ofisi ndogo za bunge kuwa ni kutaka kuwaachia wengine kushika nafasi ya uspika kutokana na yeye kulitumikia taifa kwa miaka 40 lakini si hoja nzito sana.

Ingawa sifa za kiongozi wa ngazi hiyo zimeainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari MwanahalisiONLINE limegundua kuwa kuna umuhimu wa spika huyo kuwa na sifa za ziada, mbali na zilizoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo wachunguzi wa siasa za Tanzania wamedai kuwa Makinda amekuwa spika wa bunge hilo kwa kigezo cha ujinsia kilichowekwa na CCM na sio uchapakazi kigezo ambacho kinadaiwa kuwa kilichomekwa na wanamtandao wa Kikwete ili kumwondoa Sitta katika kinyang’anyiro cha mwaka 2010.

Makinda ameonyesha udhaifu wake wakati wa vikao vya bunge la 10 baada ya kuhenyeshwa na Kambi ya upinzani hasa Mbunge wa Singida mashariki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lissu na Mbunge mteule wa jimbo la Kibamba kwa tiketi ya chama hicho, John Mnyika.

Wabunge hao walimuuliza maswali mengi ambayo Makinda katika nyakati tofauti alilazimika kuahirisha vikao vya bunge mara kwa mara.

Makinda amewaambia waandishi wa habari wiki hii kuwa kwa aina ya wabunge waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu, utaona kuna mchanganyiko wa vijana na wengi wao wakiwa wageni bungeni, sasa ni vyema Spika atakayechaguliwa alijue hilo. Na huenda likawa ni jambo la pili lililopelekea kukacha nafasi hiyo.

“Pamoja na wabunge waliokuwepo kwenye bunge lililopita kuingia tena bungeni, lakini uwepo wa vijana na wabunge wapya wengi, utaleta changamoto bungeni, kwani wananchi hivi sasa wamechagua wabunge wanaowaona ni wachapa kazi,” alisema.

error: Content is protected !!