Monday , 22 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makinda aipigia debe serikali ya JPM kanisani
Habari Mchanganyiko

Makinda aipigia debe serikali ya JPM kanisani

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda
Spread the love

MWENYEKITI wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, amewataka Watanzania kutorubuniwa na baadhi ya wanasiasa kuwa hali ngumu ya uchumi inasababishwa na mtu bali ni hali ya kidunia, anaadika Mwandishi Wetu.

Akisalimia waumini baada ya Misa ya pili ya shukrani ya Padre mpya Damian Ndege, aliyepata upadrisho, Julai 13, mwaka huu, iliofanyika Jimbo Kuu la Arusha St. Theresia, Makinda anasema anasikitishwa kusikia Watanzania wanadanganywa kuwa hali ngumu ya uchumi inasababishwa na mtu fulani, wakati hata Marekani hali nayo ni ngumu.

Hivi sasa baadhi ya wanachi wamekuwa wakiilamu serikali ya Rais John Magufuli kuwa imesababisha ugumu wa maisha.

“Jamani hakuna mtu yeyote aliyesababisha  hali hii tuliyonayo bali ni hali ya kidunia, Marekani kwenywe mtu akidondosha dola 10, anahangaika kuitafuta, hivyo ni hali ya kidunia tusidanganyike na wanasiasa au watu wanaopita pita kusema ni mtu fulani kasababisha, lakini haizuii kilamtu atafsiri atakavyo,” alisema.

Aliwaomba waumini hao na Watanzania kupitia Misa hiyo, kuwa vema kila mmoja akafanya kazi na akipata fedha yake aipangilie kufanyia vitu vya msingi na sio kuchezea.

“Kila mmoja afanye kazi kutafuta pesa na ukiipata uipangilie na sio kuichezea ule wakati wa kuchezea pesa umepita,nawaomba sana ifanyieni vitu vyamsingi,” alisema.

Aidha, anasema moja ya vitu vya msingi vya kufanyia fedha wanazopata ni kuwekeza katika Bima ya Afya, ili mtu anapougua asipate homa ya kutafuta fedha ambayo imejificha, bali atumie kadi kupara huduma.

Anasema atafurahi sana katika kipindi chake cha Mfuko huo aondoke na kuacha Watanzania asilimia 80 wanatibiwa kupitia Bima ya Afya.

“Ndugu zangu suala hili lina faida kubwa hata nchi zilizoendelea wanatibiwa kwa kadi za bima ya afya, hivyo sio sualala kulipuuzia, ifike wakati kila mmoja alibebe kwa nafasi yake na mfuko huo unapokea watu wa makundi yote,” alisema.

Pia alitumia fursa hiyo kuwasihi akina baba walevi wanaotumia hovyo fedha zao kunywa Pombe, huku familia zao zikikosa matibabu pale.

Alimalizia kusema hivi sasa kila mtu ana hali ngumu, hivyo sio wakati wa ndugu kulaumiana kuwa hawataki kusaidiana, ni vizuri kila mmoja akajiwekeza katika bima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

Habari Mchanganyiko

DCEA yakamata kilo 767.2 za dawa za kulevya, 21 mbaroni

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!