January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makete wamlalamikia mbunge wao

Mbunge wa Makete, Dk. Binilith Mahenge (aliyesimama) akiungumza na waandishi wa habari hawapo pichani

Spread the love

WANANCHI wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe wamemlalamikia mbunge wao, Dk. Binilith Satano Mahenge kwa kuruhusu miradi iliyo chini ya kiwango kuendelea katika wilaya yao. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Miradi hiyo inayodaiwa kuwa chini ya kiwango ni ujenzi wa barabara , maji na umeme ambapo wamedai, wakandarasi waliopewa kazi hiyo hawafanyi kwa ufanisi hivyo kusababisha uharibifu zaidi.

Wakiwasilisha malalamiko hayo kwa niaba ya wananchi wa Makete, kwenye mkutano wa sita wa Umoja wa Wanamaendeleo Uwanji (UDT), uliofanyika Jijini Dar es Salaam, wamemtaka Dk. Mahenge ambaye ni Waziri wa Mazingira kufuatilia miradi hiyo.

Taasisi ya UDT wilayani humo ilianzishwa kwa madhumuni ya kusaidia katika nyanja ya elimu, afya, mazingira pamoja na kufanya shughuli mbalimbali za kukuza uchumi kwenye maeneo wanayoishi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa UDT, Alnason Nguvila amesema, lengo lingine ni kutoa ushauri na elimu kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI hususan jamii ya watu wa Makete.

“Licha ya kufanya shuguli hizo, lakini bado tuna fursa ya kutoa maoni yetu na mapendekezo kwa niaba ya wananchi wenzetu, kwa mbunge na namna ya kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika wilaya yetu,” amesema Nguvila.

Akijibu malalamiko hayo Dk. Mahenge amesema, “kwa kweli kuna vitu vingine vinaendelea katika wilaya yangu na kuwa sivijui kutoka na shughili za kiserikali kuwa nyingi, lakini nashukuru kwa kuniambia na ndio raha ya uwepo wenu, tushirikiane kuvumbua maovu.”

Dk. Mahenge amewaahidi UDT kwa niaba ya wakazi wa makete, kuboresha miundombinu na miradi yote inayoendelea Makete.

Pia ametoa wito kwa wilaya zingine kuiga mfano kwa UDT ili kuweza kuwakumbusha viongozi wao pale wanapokosea katika shughuli za maendeleo.

error: Content is protected !!