Thursday , 29 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Makamu wa rais mpenda anasa atupwa jela
Kimataifa

Makamu wa rais mpenda anasa atupwa jela

Teodorin Obiang
Spread the love

MAHAKAMA nchini Ufaransa imemhukumu makamu wa rais wa Equatorial Guinea, Teodorin Obiang kifungo cha miaka mitatu jela ambacho kimeahirishwa.

Obiang 48, hufahamika sana kutokana na maisha yake ya anasa ambaye pia ni mtoto wa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Licha ya kuhukumiwa kifungo jela, lakini magari yake ya kifahari yamekamatwa.

Obiang hakuwepo mahakamani wakati mahakama ilipomkuta na hatua ya ubadhirifu wa mali ya umma.

Mali zake za Ufaransa zilichukuliwa ikiwa ni pamoja na jumba la kifahari eneo la Avenue Foch jijini Paris. Kadhalika amepigwa faini ya Euro 30m (£27m; $35m) ambayo imeahirishwa.

Obiang alikuwa ameshtakiwa kwa kutumia fedha za serikali kufadhili maisha ya anasa katika mji mkuu wa Ufaransa wa Paris.

Miongoni mwa matumizi ya fedha hizo kni pamoja na ununua majengo ya kifahari yenye kugharimu zaidi ya dola milioni 100, boti la kifahari lenye urefu wa mita 76, na magari mengi ya kifahari kama vile Bugatti, Ferrari na Rolls Royces.

Waendesha mashtaka nchini Marekani tayari walikuwa wamemlazimisha kutoa mali kadhaa likiwemo jumba lenye thamani ya milioni 30 huko California na katika maskani ya Michael Jackson.

Babake Teodoro Obiang Nguema, amekuwa madarakani tangu mwaka 1979 na ndiye rais wa Afrika aliyetawala kwa muda mrefu zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!