Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Makamu wa Rais Gambia ajiuzulu
KimataifaTangulizi

Makamu wa Rais Gambia ajiuzulu

Isatou Njie, Makamu wa Rais wa Gambia
Spread the love

ISATOU Njie, Makamu wa Rais wa Gambia ametangaza wazi kuachia ngazi hiyo kufuatia sintofahamu ya hali ya kisiasa iliyotanda katika Taifa hilo la Afrika Magharibi, anaandika Wolfram Mwalongo.

Hatu hiyo imekuja wakati tayari Mawaziri zaidi ya saba wamejiuzulu, hali hiyo imetokana na uamzi wa Rais Yahya Jammeh kutangaza wazi kwamba hawezi kuachia nchi kwa mpinzani wake Adama Barroa aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Rais Jammeh amekataa katu kuondoka Ikulu ya nchi hiyo kwakile alichodai kwamba uchaguzi uliompa ushindi mpinzani wake uligubikwa na kasoro hivyo anataka urudiwe.

Bunge la nchi hiyo limetangaza kumwongezea muda kiongozi huyo huku Wafuasi wa Barrow wakishutumu maamzi hayo kwa kile wanachodai bunge la nchi hiyo limeshindwa kusimami misingi ya sheria.

Kwa mjibu wa Shirika la habari la Al Aljazeera Adama Barrow ambaye alipaswa kuingia Ikulu ya Gambia hii leo, anatarajiwa kuapishwa ubalozini nchini Senegal.

Wakati huo vikosi vya kijeshi kutoka mataifa mbalimbali ya  Jumuhiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi (ECOWAS) vimeendelea kutia nanga kwenye Ardhi ya Gambia ikiwa ni maandalizi ya kumung’oa kwa mtuu Rais Jammeh.

Ousman Badjie Mkuu wa majeshi wa Gambia hivi sasa ameonekana kujiweka kando na Rais Jammeh kwakile alichodai kuwa hatathubutu kuruhusu majeshi yake kufanya mashambulizi kwa yeyote.

Huku akionekana kubadili msimamo wake wa awali ambapo Jenerali huyo alitangaza wazi kumuunga mkono Rais aliyemadarakani.

Wagambia wameendelea kukimbia nchi yao na kuingia nchini Senegal kwakuhofia machafuko kutokana na azma ya Wafuasi wa Barrow kumtangaza Rais Jammeh kuwa “muasi”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Rais Tshisekedi amteua kiongozi wa wanamgambo kuwa Waziri wa Ulinzi

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi,...

Kimataifa

Raila Odinga: Tutafanya maandamano makubwa mara mbili kwa wiki

Spread the love KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Amollo Odinga ametangaza...

Kimataifa

Magharibi kuwekeza silaha Indo-Pacific, China yachochea

Spread the love KUVUNJIKA ushirhikiano wa China na Magharibi uliodumu kwa takribani...

Kimataifa

Ruto amlaumu Odinga kujaribu kuanzisha mgogoro kwa mara ya pili

Spread the love  RAIS wa Kenya William Ruto amesema kwamba hatakubali “kutoijali...

error: Content is protected !!