July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Makamu Mwenyekiti NCCR atumbuliwa

Spread the love

 

LETECIA Ghati Mosore, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi Bara ameng’olewa katika nafasi hiyo pia kuvuliwa uanachama wa chama hicho, anaandika Pendo Omary. 

Amefukuzwa baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho iliyofanya kikao chake Jumamosi wiki iliyopita kubaini anakihujumu chama hicho.

Akieleza maazimio ya NEC leo, James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi amesema, “chama kinamsimamisha uongozi wa umakamu mwenyekiti ndugu Leticia Ghati  Mosore na baadaye kumvua uanachama.

“Hii ni baada ya kikao hicho kujibadilisha kuwa kamati ya nidhamu na usuluhishi ,” amesema Mbatia.

Mbatia amesema, NEC ilichukua uamuzi huo wa kumvua uanachama baada ya kujiridhisha kwamba, Mosore wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita alijihusisha na migogoro ndani ya chama, kutoa tuhuma dhidi ya viongozi wa chama au mwanachama nje ya utaratibu, kukashifu viongozi wa chama, kuhujumu chama na kutoa na kupokea rushwa.

“Kwa makosa hayo ambayo ndugu Mosore aliyatenda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Halmashauri Kuu ya Taifa, inamsimamisha uongozi na kumvua uanachama,” ameeleza Mbatia.

Aidha, Mbatia amesema, kati ya kura 61 za wajumbe zilizopigwa, kura 57 zilisema avuliwe uanachama, kura moja ilisema hapana, kura tatu hazikuwa na upande.

 

Hata hivyo amesema, wajumbe walifikia uamuzi huo kwa kuzingatia jedwali la makosa na adhabu zake; kifungu cha 2,5,6,10 na 12.

Pia, NEC imemtaka Mosore kupinga uamuzi huo kama ataona hakutendewa haki kwa kuwa, katiba ya chama hicho inatoa nafasi kwa kila mwanachama kupinga uamuzi pale atakapoona hakutendewa haki.

 

error: Content is protected !!