May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makamo wa  Kwanza wa Rais Zanzibar, athibitika kuugua Corona

Maalim Seif Sharrif Hamad, Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Spread the love

 

MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amepata maambukizi ya virusi hatari vya Corona (Covid 19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa kutoka Zanzibar na makao makuu ya chama cha ACT- Wazalendo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, zinasema kuwa Maalim Seif pamoja na mkewe, Bi. Awena wamepata maambuzi hayo na wote wawili, wamelazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, Unguja.

Wengine waliothibitika kuambukizwa virusi hivyo, ni wasaidizi kadhaa wa kiongozi huyo, maarufu Visiwani.

Maalim Seif alianza kujisikia vibaya mwishoni mwa wiki iliyopita, ambako Jumanne iliyopita, akafanyiwa vipimo vya Covid 19 na kuthibitika kuwa amepata maambukizi.

“Mimi na mama yenu (Bi. Awena) baada ya kupata nimonia kali. Jumanne tukapimwa; na rapid test ilionesha viashiria kwa kuwepo kwa Covid 19. Nikashauriwa mimi na Bi Aweina tuji- self isolate tukianza kupata madawam” anaeleza Maalim katika ujumbe aliyotumwa kwa baadhi ya watu.

Maalim anasema, “…nimepata matatizo ya kupumua. Hivyo mnamo saa 11.45 jioni nimelazwa Mnazi Mmoja kwa uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi.”

Madaktari wamejitahidi sana. Sasa sijambo na matibabu yanaendelea.

Anasema, mkewe wake, amejifungia nyumbani na anaendelea vizuri na kuongeza, “musiwe na wasi wasi. Zidisheni dua tu. Mungu ataninyanyua, Amin.”

Naye Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Ado Shaibu ameeleza katika taarifa kwa umma, leo Jumapili, tarehe 31 Januari 2021, kuwa Maalim amewekwa kwenye uangalizi maalum wa madaktari katika kipindi chote atakachoendelea na matibabu.

Katika andishi lake kwa umma, Ado anasema, “Chama cha ACT- Wazalendo, kinajulisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma kwa ujumla kwa ujumla, kwamba mwenyekiti wake wa taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, mkewe Bi. Awena, pamoja na wasaidizi wake kadhaa, wamethibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.”

Bi Awena, mke wa Maalim Seif Sharrif Hamad

Anasema, “katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi, madaktari wamemshauri Maalim Seif awepo chini ya uangalizi Maalum katika kipindi hiki.”

Kupatikana kwa taarifa kuwa kiongozi huyo wa pili kwa ukubwa kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), amepata maambukizi ya Virusi vya Corona, kumekuja katika kipindi ambacho viongozi kadhaa wa madhehebu ya kidini nchini Tanzania, wakitoa wito kwa waumini na waamini wao, kujikinga na virusi hivyo.

Akizungumza katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya Kumbukumbu ya Wafia Dini, iliyofanyika katika kituo cha Hija Pungu, jijini Dar es Salaam, Askofu Mkuu Mwandamizi wa  Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi alisema, “Korona haijaisha. Tusali na tujiombee sisi wenyewe, ili Mungu atulinde na janga la Covid-19.”

Alisema, “tusiende holela. Tuwe makini na tujilinde. Utamaduni wa barakoa tuliouacha, tuurudie. Tujijali, tujipende, tujitunze, tushirikiane na Mungu katika kujilinda na tuendelee kuomba ulinzi kwa ajili yetu sote.”

Naye Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Aman ameeleza katika andishi lake alilolipa kichwa cha maneno: “Kutembea Pekupeku Juu ya Mbigili,” kuwa “…tusimjaribu Mungu kwa kufanya uzembe na maisha yetu.”

Askofu Amani alisema, “turejee  na tahadhari za kuzuia maambukizi bila ya kuwa na hofu.” Akaongeza, “tusipuuze sharti la kujikinga. Tuchukue tahadhari kwa kuwa ugonjwa huo bado upo na unatesa mataifa mengi duniani.”

Kwa upande wake, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Gervas Nyaisonga alieleza katika barua yake kwa Mwadhama, Mpelekwa wa Baba Mtakatifu, Maaskofu Wakuu, Maaskofu na Maaskofu Wastaafu, kuwa  “Tanzania siyo kisiwa.”

Alisema, “wahenga wanasema, mwenzio akinyolewa wewe wewe tia maji. Ni muhimu tukaendelea kuzingatia kanuni za afya katika kukohoa au kupiga chafya na kuepuka kusogeleana, kugusana na kusongamana.”

Barua ya rais wa TEC kwenda kwa viongozi hao, ilitumwa tarehe 26 Januari 2021 na kupewa kichwa cha maneno kisemacho, “tahadhari juu ya maambukizi mapya ya virusi vya Korona na ugonjwa wa Uviko 19 (COVID 19.”

Nyaisonga ni Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya.

Alisisitiza kuwapo wimbi jipya la maambukizo ya Korona kufuatia nchi kadhaa kuthibitisha kupita kwenye kipindi kigumu cha kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.

error: Content is protected !!