December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makamishna wapya, maafisa waandamizi Tume za Uchaguzi SADC wafundwa

Spread the love

 

JUKWAA la Tume za Uchaguzi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (ECF-SADC) kwa kushirikiana na Taasisi ya International IDEA imeanza kutoa mafunzo kwa makamishana wapya na maofisa waandamizi wa tume za uchaguzi. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku nne yameanza leo Jumatatu tarehe 22, Novemba, 2022, jijini Dar es Salaam yakihusisha maafisa waandamizi na makamishna wapya 50 kutoka nchi 9 wanachama wa ECF-SADC.

Akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Jacobs Mwambegele amesema wajumbe wa mafunzo hayo watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yatakayowasaidia kuboresha utekelezaji wa majukumu yao.

Pia amesema watajifunza na kubadilishana ozoefu wa namna ambayo uchaguzi umekuwa ukifanyika katika nchi zao na kuona changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza na namna ya kuzitatua.

Jaji Mwambegele ametaja mada zitakazowasilishwa katika mafunzo hayo kuwa ni pamoja na demokrasia, uchaguzi na menejimenti ya uchaguzi; vigezo vya kimataifa vya upimaji wa uchaguzi na wajibu wa kuendesha chaguzi za kidemokrasia; usimamizi wa uchaguzi, mifumo ya uchaguzi, mzunguko, kalenda na mipango ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Jacobs Mwambegele

Mada zingine ni pamoja na matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi; masuala yanayojitokeza katika usuluhishi wa migogoro ya uchaguzi na utoaji hai katika uchaguzi; uandikishaji wa wapiga kura; siku ya uchaguzi na menejimenti ya matokeo; changamoto kwa Tume za Uchaguzi na uongozi wa Tume za Uchaguzi, utendaji kazi na uendelevu wake.

Zingine ni kuendesha uchaguzi jumuishi kwa kuzingatia jinsia, vijana na watu wenye ulemavu; menejimenti ya mashinikizo ya kisiasa; kugharamia uchaguzi na Tume za Uchaguzi ushirikiano wa Tume za Uchaguzi na vyombo vya habari, kukabiiana na majanga na usalama wakati wa uchaguzi .

“Baada ya kupatiwa mafunzoi ni matarajio kuwa watendaji hawa waakwenda kuhakikisha kuwa chagzui zinakuwa huru, za haki na zenye kuaminika. Hii itasaidia katika kukuza demokrasia itakayochochea amani, usalama na ustawi wa wananchi na Taifa,” amesema Jaji Mwambegele.

Naye Mwwenyekiti wa Kamati Tendaji ya ECF-SADC ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Namibia, Bi Elsie Nghikembua, amesema uzoefu wa nchi za SADC na Afrika kwa ujumla unaonesha kuwa menejimenti za uchaguzi ambazo zinafuata taaluma na kutokuwa na upande ni muhimu katika kufanya uchaguzi unaoaminika.

“Ili chaguzi ziende vizuri zinahitaji kufanyika kwa uaminifu na kuakisi kile wananchi walichochagua,” amesema Bi Nghikembua.

Amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuwapa utaalamu, kanuni na misingi mzuri ya kuendesha chaguzi na kuwapa maarifa muhimu katika majukumu yao mapya.

Katika hatua nyingine Bi Nghikembua ametaja changamoto zinazowakabili kama wasimamizi wa uchaguzi ikiwemo ufinyu wa bajeti, upungufu wa mafunzo na kuingiliwa na mamlaka za kimataifa.

Jukwaa hilo lilianzishwa rasmi Julai 1998 nchini Botswana kwa lengo la kuchagiza uwepo wa Tume Huru za Uchaguzi katika ukanda huo.

error: Content is protected !!