Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Michezo Makambo ruksa kuivaa USM Alger
Michezo

Makambo ruksa kuivaa USM Alger

Heritier Makambo
Spread the love

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Heritier Makambo amepewa ruhusa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika ‘CAF’ kuitumikia klabu hiyo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaofanyika tarehe 19 Agosti, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Hapo awali uongozi wa klabu hiyo ulipeleka majina ya wachezaji watatu kwenye shirikisho hilo ambao ni Deus Kaseke, Matheo Antony na Heritier Makambo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao baada ya kufanikiwa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuanio hiyo huku kanuni zikiwaruhusu kufanya hivyo.

Yanga yenye alama moja ambayo inashika nafasi ya mwisho kwenye kundi D baada ya kucheza michezo minne, huku ikipoteza michezo mitatu na kwenda sare mmoja, hivyo kupoteza matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuani hiyo.

Katika mchezo ujao dhidi ya USM Alger utakuwa kipimo tosha kwa mshambuliaji huyo raia wa DR Congo ambaye ameingia kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili, huku likiwa pendekezo la kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera ambaye atakiongoza kikosi hicho katika msimu ujao wa mashindano.

Katika hatua nyingine klabu hiyo inatarajia kucheza mchezo maarumu wa kirafiki kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ametundika daruga, kwenye uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

error: Content is protected !!