August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makamba: Serikali imejiandaa kukabili mazingira

Spread the love
SERIKALI imeandaa mkakati wa kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi, anaandika Regina Mkonde.
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi wa Jumuiya ya Kimataifa Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano amesema, serikali imeandaa miradi mitano itakayosaidia kuondoa changamoto hizo.
“Lengo la kuitisha mkutano huu na wadau ni kujadili juu ya utekelezaji wa miradi mitano iliyolengwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2020) ni kuhakikisha kuwa changamoto ya uharibifu wa mazingira inapungua,” amesema Makamba.
Ameitaja miradi hiyo kuwa pamoja na mradi wa kuwezesha Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifala Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na serikali kutekeleza sera ya mazingira kwa kuipa uwezo wa kifedha na upandaji wa miti katika kila kijiji na maeneo yaliyo wazi.
“Mradi wa upandaji miti utafanyika ndani ya miaka mitano,  tumepanga kutumia bilioni 5  ambapo tutatengeneza vitalu na mfumo wa ugawaji miti pamoja na kuitunza hadi kukua kwake,” amesema.
Makamba amesema kuwa, mradi huo utahusu kuwezesha kiuchumi mfuko wa taifa wa mazingira ambao kwa miaka 10 ulishindwa kufanya kazi kutokana na uhaba wa fedha.
Amesema, takribani hekari nane zinapotea kutokana na uharibifu wa mazingira unaosababisha unyeshaji wa mvua kupungua.
“Ili kuepukana na tataizo la mabadiliko ya tabia ya nchi hatuna budi kuitunza misitu na kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia nishati mbadala kwa kushusha gharama za gesi,” amesema.
error: Content is protected !!