Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Makamba atangaza masharti ununuzi nguzo za umeme ndani
Habari Mchanganyiko

Makamba atangaza masharti ununuzi nguzo za umeme ndani

Spread the love

WAZIRI wa Nishati, January Makamba, ameagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), liingie zabuni za ununuzi wa nguzo za kusambazia umeme kwa wakandarasi watakaokidhi vigezo, ikiwemo kuthibitisha kuwa baadhi ya nguzo hizo zimetoka kwa wazalishaji wadogo wa ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Makamba ametoa maagizo hayo leo Jumamosi, tarehe 30 Aprili 2022, mkoani Iringa, akizungumza na wadau wa uzalishaji nguzo nchini.

“Tutakapotoa zabuni ili ufanikiwe lazima walau asilimia fulani ya hizo nguzo utakazouza ziwe zimetoka kwa watu wadogo wadogo. Katika nyaraka yako ya kuomba zabuni ili ufanikiwe lazima uthibitishe asilimia 20 au 10 inatoka kwa wadogo na uwe na mikataba nao,” amesema Makamba.

Aidha, Makamba ameiagiza TANESCO, ishirikiane na taasisi zinazosimamia ubora wa bishaa, ikiwemo Shirika la Viwango nchini (TBS), ili kuhakikisha nguzo zinazonunuliwa zinakidhi viwango hivyo.

Aidha, Makamba amesema ataunda kamati ya wadau watakaofuatilia namna ya utengenezaji nguzo bora za umeme, ambao baadhi yao watapelekwa nje ya nchi kujifunza kuhusu suala hilo ili wapate uzoefu.

“Sasa ipo mifano ya mfumo huu wa uwekaji, nchi ya South Afrika ina mfumo, sisi tuko tayari kuchukua watu kadhaa kwenye kila wadau kuwapeleka na kuwalipia mkajifunze khusu mfumo wa kudhibiti na kuhusu ubora,” amesema Makamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!