November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makamba amtumia ujumbe Rais Magufuli

Spread the love

JANUARY Makamba, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), amemtumia jumbe Rais JohnMagufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Muda mfupi baada ya Rais Magufuli kumwapisha George Simbachawene kuongoza wizara ya Muungano na Mazingira, Makamba amemtumia kiongozi huyo wa nchi kupitia ukureasa wake wa twetter leo tarehe 22 Julai 2019.

Kwenye ujumbe wake huo Makamba amesema, anamshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini na kumpa nafasi ya kutumikia Watanzania katika serikali yake.

Kwenye ujumbe huo Makama ameelekeza shukrani zake kwa Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais pamoja na Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu.

Makamba ameandika “Neno la Mwisho kwenye hili: Namshukuru Rais kwa kuniamini, Makamu wa Rais kwa kunielekeza, PM kwa kunisimamia, na Team ya VPO/NEMC na Mawaziri wote kwa ushirikiano.”

error: Content is protected !!