MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla leo tarehe 28 Januari 2023 ameongoza zoezi la usafi wilayani ya Temeke katika eneo la Mbagala na kupiga marufuku kufanya biashara kwenye ujenzi wa barabara ya mwendokasi na maeneo yaliyokatazwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Makalla ametumia zoezi hilo kuwakumbusha wananchi na viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi wilaya kuhakikisha wanasimamia usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Aidha RC Makalla amewaelekeza Wakurugenzi kusimamia wakandarasi kuondosha taka kwa wakati na wale watakaoonyesha kulegalega wasipatiwe mkataba.
Pia amewapongeza wananchi kufanya usafi jambo lililopelekea Jiji la Dar es salaam kushika nafasi ya sita kwa usafi Barani Afrika na kuondosha magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam, zaidi ya Sh bilioni 3.2 zimetolewa kama mkopo kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara kwenye maeneo rasmi na kutoa wito kwa wafanyabiashara wengine kuacha kufanya biashara holela.
Leave a comment