Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Makala atoa mwezi mmoja kwa machinga kupangwa upya
Habari Mchanganyiko

Makala atoa mwezi mmoja kwa machinga kupangwa upya

Wafanyabiashara wa Soko a Kariakoo waliohamia kwenye Soko la Machinga Complex wakiwa juani kutokana na eneo hilo kutokuwa na paa
Spread the love

 

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ametoa muda wa mwezi mmoja kwa madawati ya uwezesha wananchi kiuchumi yaliyopo katika kila wilaya kuanza maandalizi ya kuwapanga upya na vizuri wafanyabiashara wadogo ‘wamachinga’ kuanzia Jumatatu tarehe 20 Septemba hadi tarehe 18 Oktoba, 2021. Anaripoti Patricia Kighono na Noela Shilla, TUDARCo … (endelea).

Makalla ametoa tamko hilo leo tarehe 17 Septemba 2021 wakati akizindua kitabu cha mpango wa kuwapanga vizuri wafanyabiashara hao jijini Dar es salaam.

Makalla amesema uwepo wa machinga katika maeneo hayo yasiyorasmi umekua na athari nyingi ikiwemo kusababisha msongamano wa watu, ajali, kuikosesha serikali mapato na hata kukwamisha juhudi za mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO – 19.

Makalla amesema mpango huo umewashirikisha wadau wote ikiwamo wafanyabiashara hao jambo lililowawezesha kujua wapo wangapi katika kila wilaya.

Aidha, aliyataja makundi matano ambayo mpango huo utawagusa kuwa ni wafanyabiashara waliojenga vibanda juu ya mifereji na mitaro, wale walio mbele ya maduka ya watu na kusababisha wateja kushindwa kuingia na kutoka dukani.

Amos Makala, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam

“Wafanyabiashara waliopo katika hifadhi za hifadhi ya barabara yaani road reserve, wanaofanya biashara na kuzuia njia za waenda kwa miguu hali inayolazimu baadhi kugongwa na magari kwa kupita barabara kabisa na wale wanaofanya biashara mbele ya taasisi za umma, shule za msingi na sekondari,” amesema.

Aidha, ameiagiza ofisi ya mkuu wa mkoa kuendelea kuweka mabango ya katazo ya kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.

Amesema kila mkuu wa wilaya kuhakikisha madawati hayo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, yanaratibu wamachinga hao bila bughdha.

Aidha, Mwakilishi wa wamachinga, Steven Lusinde ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania, amesema utaratibu huo wa mkuu wa mkoa ni mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine.

“Tumepokea agizo lako tutalifikisha kwa wenzetu kama lilivyo ili kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakuu wa wilaya.

“Tunaomba wakuu wa wilaya wazingatie hili kwamba kutupanga upya na kutupanga vizuri, kwa sababu kuna maeneo wanastahili kutupanga vizuri maana tupo maeneo sahihi na si upya,” amesema.

Amesema ni kweli wamachinga wamekiuka utaratibu kwa kufanya biashasha maeneo yasiyorasmi.

“Niwaombe wenzangu popote walipo nikiwa kama makamu mwenyekiti wa machinga Tanzania kwamba kwa maelekezo haya tuwe watulivu tuhakikishe tunajipanga vizuri,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!