January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makada wa Chedema wapata dhamana

Vijana wa Chadema waachiwa kwa dhamana

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika (mweye mawani) akiwa pamoja na vijana wa Chadema waliokuwa wakishikiliwa na polisi, muda mchache baada ya kuachiwa kwa dhamana

Spread the love

WANACHAMA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaotuhumiwa kumteka na kumtesa aliyekuwa mlinzi wa Katibu wa chama hicho, Dk. Willibrod Salaa, aitwaye Khalidi Kangezi wameachiwa kwa dhamana. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Washtakiwa hao diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob, Mlinzi Hemed Sabula na Afisa Utawala wa chama hicho, Benson Mramba, wanatetewa na mawakili Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

Dhamana hiyo imetolewa leo saa 11:00 jioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema, baada ya washtakiwa kutimiza masharti ya dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja ambao wanatoka katika taasisi inayotambulika au serikalini isipokuwa walimu na kusaini hati ya dhamana ya sh. 10 milioni.

Akizungumza kwa niaba ya washitakiwa wenzake, Jacob amesema “tumetoka ndani. Tunajipanga ni namna gani ya kutoa ushahidi wa kumuua Dk. Slaa”.

“Kabla hatujakamatwa na kuwekwa mahabusu ushahidi uliotoka awali ulikuwa ni robo tu. Hawawezi kutuweka ndani milele. Tutapata nafasi na kuwajulisha watu kuhusu mkakati mbaya wa Usalama wa Taifa na Chama Cha Mapinduzi kuhusu kudhuru maisha ya Dk. Slaa,” amesema Jacob.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Myika aliyekuwa mahakamani hapo tangu saa mbili asubuhi kufuatilia dhamana hiyo, amesema, kitendo cha wahalifu kulidwa huku raia mwema anayehakikisha taarifa ya njama za mauaji anageuziwa kesi kinaashiria kuna ubaguzi.

“Sisi viongozi tunapokea malalamiko. Kumbe polisi hawako tayari kuwahoji watuhumiwa waliokula njama za kumuua Dk. Slaa. Kuhusu Kova- kutangaza kufungua mafaili hayo ni ya polisi sio ya mahakama. Wanatakiwa kutambua kwamba wananchi na wanachama wa Chadema wako tayari kuchukua hatua wanazoona zinafaa,” amefafanua Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Ubungo.

Katika kesi hiyo namba 54 ya mwaka 2015, watuhumiwa wanashtakiwa kwa kosa la kumjeruhi Kangezi  mnamo tarehe 7 Machi mwaka huu.

Katika shtaka hilo washtakiwa wanadaiwa kwamba tarehe hiyo wakiwa Makao Makuu ya Ofisi za Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Dar es Salaam, walimjeruhi Kangezi kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali. 

Ingawa Wakili wa Chadema, John Malya alimfikisha Kangezi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay na kumfungulia shitaka la kupanga njama za kumuangamiza Dk. Slaa kwa kumuwekea sumu kwenye maji au chakula  lakini Kagezi bado yupo nje huru.

Pia wanaotuhumiwa katika njama hizo za kutaka kumua Dk. Slaa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula hawajafunguliwa mashtaka. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 26 mwaka huu.

error: Content is protected !!