Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makada CCM 8 wapitishwa kuwania ubunge EALA
Habari za SiasaTangulizi

Makada CCM 8 wapitishwa kuwania ubunge EALA

Spread the love

WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana wamewachagua wagombea nane kati ya 26 watakaokwenda kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) tarehe 22 Septemba, 2022 bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu (endelea).

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Kamati Kuu ya CCM (CC) katika kikao kilichoketi jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, tarehe 7 Septemba, 2022, kuteua na kupendekeza majina 26 ya makada hao ambao jana tarehe 10 Septemba, 2022 wamechujwa na wabunge wa CCM na kubakia nane.

Waliochaguliwa ni; Dk Ng’waru Maghembe, James Millya, Anar Kachwamba, Dk Shogo Mlozi, Angela Kizigha, Machamo Ali Machamo, Dk Abdulla Hasnuu Makame na Nadra Juma Mohamed.

Katika Bunge la Eala, Tanzania ina nafasi tisa na kati ya hizo nane ni za Chama Cha Mapinduzi na moja ya vyama vya upinzani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!