August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makada 6 Chadema waliokaa mahabusu miaka 3 waachiwa huru

Spread the love

HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imemuachia huru aliyekuwa diwani wa Chadema katika Kata ya Isengule wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi, Oscar Sangu na wenzake watano baada ya kukaa gerezani kwa tuhuma za mauaji kwa zaidi ya miaka mitatu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Katavi … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 4 Agosti, 2022 mkoani Katavi na Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na MwanaHalisi Online, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi na Wakili Gaston Shundo Garubindi amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya upande wa Jamhuri kuonekana hawana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Wakili Garubindi amewataja makada hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa Diwani wa Kata Isengule, Oscar George Sangua.

Wengine ni Emannuel Sebastina John, Respic Julius Namwala, Busiga Clement, Januari Katuhu, Mickson Makatale ambao wote kwa pamoja walituhumiwa kwa makosa ya mauaji.

Amesema makada hao walituhumiwa kwa muaji yaliyotokea  tarehe 23 Juni, 2019 katika Kijiji cha Kasangatonge Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi baada ya kutokea mauaji kijijini hapo ambapo aliyekuwa diwani ambaye alikuwa mshtakiwa namba moja walikamatwa katika sakata hilo na kushtakiwa kwa kosa la mauaji.

Wakili Gaston Shundo Garubindi

“Walikuwa ndani tangu mwaka 2019 lakini leo mwaka 2022 hatimaye mahakama kuu wameachiwa huru baada ya Jamhuri kuonekana hawana nia ya kuendelea na shauri hilo.

“Kwa hiyo viongozi na wanachama wetu wamekaa ndani zaidi ya miaka mitatu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba hatimaye haki imeonekana, imetendeka na sasa viongozi hawa wamerudi uraiani kuungana na familia zao.

“Na sasa wanarejea uraiani kutokana na maamuzi, hayo tuendelee kusukuma gurudumu letu la maisha ambalo kwa kipindi kirefu walikuwa wameshikiliwa, tunawakaribisha sana uraia maisha mengine yaendelee,” amesema.

Amesema kesi ya mauaji haikuwa na hukumu kwa sababu ya mchakato wake wa usikilizwaji wa awali katika mahakama ya chini ulianza kwa kukusanyaji wa vielelezo.

“Kwa hiyo mahakama ya chini haiwezi kusikiliza mauaji, ilipelekwa mahakama kuu ndipo kesi namba 28 ya mwaka 2019 ilipofikia tamati leo,” amesema.

error: Content is protected !!