December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Makaburi Pwani, Moro kuhamishwa kupisha Standard Gauge

Spread the love

SHIRIKA la Reli nchini (TRC) linatarajia kuhamisha makaburi kwenye mikoa ya Pwani na Morogoro ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa ‘Standar Gauge. Anaripoti Mwandishi Wetu …. (endelea).

Tangazo la uhamisho wa makaburi hayo limetolewa leo tarehe 24 Oktoba 2018 na Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Reli nchini (TRC). Ambapo limetaja kuwa, makaburi hayo  yako ndani ya Halmashauri za Wilaya ya Kisarawe, Kibaha na Morogoro.

Kwa mujibu wa TRC, uhamisho huo utaanza kutekelezwa siku saba baada ya tangazo lake kutolewa.

“Katika halmashauri ya wilaya ya Kisarawe zoezi litafanyika kwenye kitongoji cha Kisarawe eneo la Mwambisi,  kwa upande wa Kibaha Vijijini litafanyika vijiji vya Soga, Magindu, Ngeta, Kikongo, Minazi Mikinda. Halmashauri ya wilaya ya Morogo uhamisho utafanyika vijiji vya Mgude, Mikese, na Mtego wa Simba.

Wakati Masnispaa ya Morogoro uhamisho utafanyika mtaa wa Seminari, Tungi, Kambi Tano na Tushikamane,” imeeleza TRC.

TRC imewataka wasimamizi wote kufika katika ofisi za maafisa watendaji wa vijiji na mitaa wa maeneo husika wakiwa na nyaraka zinazo watambulisha.

error: Content is protected !!