Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Makabila mchanganyiko kikwazo cha usafi Dar – Meya Moshi
Habari Mchanganyiko

Makabila mchanganyiko kikwazo cha usafi Dar – Meya Moshi

Moja ya sehemu chafu wa jiji la Dar es Salaam
Spread the love

MEYA wa Halmashauri ya Mji Moshi, Raymond Mboya amesema, mchanganyiko wa makabila katika Jiji la Dar es Salaam ni miongoni mwa vikwazo katika kutatua kero ya usafi. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online ofisini kwake Moshi, Mboya ambaye ni Diwani wa Kata ya Longuo amesema, mji huo umefanikiwa kuwa msafi kutokana na elimu waliyopatiwa wananchi.

Na kwamba, uelewa walionao wakazi wa mji huo ni mkubwa ukilinganisha na wakazi wa Dar es Salaam kutokana na jiji hilo (Dar es Salaam) kuwa na mchanganyiko wa makabila huku kila moja lina utamaduni wake.

Mboya amesema, kutokana na mchanganyiko huo, umesababisha uongozi wa jiji hilo huo kupata shida katika kuhakikisha unakuwa safi.

“Dar es Salaam unaweza kupanga nyumba na ukawa mstaarabu na ukawa na elimu ya usafi wa mazingira, lakini utashangaa mwenzako anaweza akamwaga maji machafu mbele ya nyumba yake akaona ni kitu cha kawaida hivyo inachukua muda mrefu kumbadilisha mtu,”amesema.

Hata hivyo amesema kuwa, Halmashauri ya Mji wa Moshi wamejiwekea utaratibu maalum, ambao unamfanya mwananchi kutambua na kupokea elimu wanayopewa juu ya mazingira na miundombinu na kuwa, wameweka faini hata kwa anayetema mate.

“Moshi huwezi kumkuta mama ametoka jikoni na maganda ya vitunguu akamwaga mbele ya nyumba yake, hiyo kitu Moshi hakuna kwasababu watu wana uelewa wa kutosha kuhusu mazingira, nawapongeza watu wa Moshi. Moshi imekuwa ikiongoza kwa miaka mingi,” amesema.

Kuhusu mradi wa Soko Kubwa na Stendi katika mji huo Mboya amesema kuwa, wapo katika hatua nzuri za ujenzi huo ambapo hapo nyuma ilichukua muda kutokana na waziri aliyekuwa wa TAMISEMI, George Simbachawene kukwamisha miradi, hivyo baada ya kuwekwa Selemani Jafo ujenzi huo umeenda vizuri.

“Kwa sisi tulikuwa tunaona Simbachawene alikuwa anakwamisha maendeleo, lakini tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kumuweka Jafo ili aendane na spidi yake na ametupa kibali tumeanza ujenzi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!