Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Makabidhiano ya dhahabu yamkwamisha Mbowe, wenzake 
Habari za Siasa

Makabidhiano ya dhahabu yamkwamisha Mbowe, wenzake 

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo tarehe 24 Julai 2019 imeahirisha kusikiliza kesi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Sababu za kuahirishwa kesi hiyo, ni kutokana na mawakili wa serikali kuhudhuria hafla makabidhiano ya kilogramu 35 za dhahabu kati ya Tanzania na Kenya.

Viongozi wa Chadema wanaokubaliwa na kesi hiyo ni pamoja na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa;  Vicent Mashinji, Katibu Mkuu;  Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Z’bar na John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara.

Wengine ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini; Ester Matiko, Mbunge Tarime Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini.

Thomas Simba, hakimu wa mahakama hiyo ameamua kuahirisha shauri hilo ambalo lililetwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi pingamizi la utetezi juu ya kupokelewa kwa kielelezo cha kamera ya video na tepu mbili za kurekodia, kilichotolewa na upande wa mashtaka tarehe 12 Julai 2019.

“Nimesikiliza upande wa mashtaka juu ya kuahirishwa kwa kutolewa uamuzi pia nimesikiliza pingamizi la utetezi.

Hakimu Simba amesema, sababu zilizotolewa juu ya ahirisho la kesi hilo haziathiri upande wowote katika kesi hii.

“Kwa maoni yangu, sababu zilizotolewa ni za msingi, kwasababu hizo mahakama inaahirisha kesi hiyo mpaka kesho saa nne,” amesema Hakim Simba.

Katika kesi hiyo, upande wa serikali uliwakilishwa na Wakili Salim Msemo huku upande wa utetezi unaongozwa na Profesa Abdallah Safari, akisaidiwa na Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya, John Mallya na Hekima Mwasipu.

Awali, wakili Msemo ameieleza mahakama kuwa upande huo umewasilisha barua iliyoitaarifa mahakama hiyo kuwa, mawakili wanaoendesha kesi hiyo ndio waandalizi wa wa tukio hilo la makabidhiano ya dhahabu hizo.

“Timu ya waandesha mashtaka ni sehemu ya waandaaji wa tukio hilo lakini pia ni sehemu ya wahudhuriaji wa tukio hilo, kwasababu hizo kama tulivyoomba kwenye barua yetu tunaiomba mahakama yako kuahirisha kutoa uamuzi mpaka kesho,” amewasilisha Msemo.

Profesa Safari amedai “timu inayoendesha mashtaka haya ina wanasheria wanne wa serikali, tukio la kupokea dhahabu sio geni, tunaahirisha kesi kwasababu Serikali ya Kenya inakabidhi dhahabu ni dharau kwa muhimili wa mahakama,” ameeleza.

Prof. Safari ameeleza kuwa, kesi hiyo inawakabili wabunge walioacha shughuli zao za kibunge kwa ajili ya kutii wito wa mahakama.

“Wabunge wameacha kazi zao za kibunge, tulikuwa na tukio la kumwaga Jaji Othaman Chande, Mahakama ya Rufaa, mimi na Prof. Issa Shivji tulialikwa, nikaomba ruhusa lakini kesi haikuarishwa, wenzangu waliendelea.

“Ingekuwa kituko kuaharisha tukio hili zito eti kisa Profesa Safari amekwanda kumwaga Jaji Chande, majaji wakuu walikuwepo majaji wote walikuwepo.

“Hawa ama ni wavivu au watatoa kisingizio cha kwenda kunywa soda, kule kwanza kuna uamuzi huyu kijana si yupo apokee uamuzi kisha aende kunywa soda. Sisi tunapinga, tuendelee na kesi hapa kama huyu hawezi basi tutaendelea kesho,” amesema.

Mawakili waandamizi wa Serikali waliohudhuria kwenye shughuli hiyo ya makabidhiano ya dhahabu ni pamoja na Faraja Nchimbi, Paul Kadushi , Wankyo Simon na Dk. Zainab Mango.

Kibatala amesisitiza, uamuzi usomwe leo ili kesho mambo mengine yote yafanywe kesho. Shauri hilo limeahirishwa mpaka kesho Alhamis tarehe 25 Julai 2019 saa nne asubuhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!