July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majimbo ya Upinzani yamtoa roho Makonda

Paul Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewachongea wabunge wa upinzani, kwa Rais John Magufuli, kwamba hawafanyi kazi za wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mbele ya Rais Magufuli, Makonda amedai kwamba, Saed Kubenea (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), John Mnyika (Kibamba) wanakula posho bungeni, pasipo kufanya kazi za wananchi.

Makonda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika hafla ya upokeaji ndege mpya ya serikali, leo tarehe 26 Oktoba 2019 jijini Dar es Salaam.

Makonda ameeleza kuwa, katika kitu ambacho wananchi wa jiji la Dar es Salaam walikosea, ni kuwachagua wabunge hao kuwawakilisha.

“Bahati mbaya sana tuna majimbo matatu tulikosea wananchi wa Dar es Salaam, jimbo la Kibamba, Ubungo na Kawe, wabunge hawa si kwamba watumishi wa nchi, ni wezi wanaokula posho bungeni bila kufanya kazi, “ amedai Makonda na kuongeza;

“Wilaya ya Ubungo ni mpya na ina wabunge wawili na meya wa upinzani,  kuja kwenye shughuli za maendeleo lakini hawawezi. Naomba nitoe kilio cha wana Ubungo ikikupendeza usikilize kilio chao. Naomba unisaidie 1.5 bilioni, niwajengee hospitali wananchi wa Ubungo.”

Wakati Makonda akitoa kauli hiyo, hivi karibuni Kubenea alilalamika kuzuiwa kufanya shughuli za maendeleo jimboni mwake na serikali.

error: Content is protected !!