August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maji yatesa Wananchi Ukerewe

Wananchi wakiwa kaitka sehemu yemye Uhaba wa maji

Spread the love

WAKAZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, wameitupia lawama Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushindwa kuwafikishia huduma ya maji safi na salama na kuwapimia ardhi kwa kipindi cha miaka 20. Anaandika Moses Mseti…(endelea).

Wananchi hao wamesema, kitendo hicho kimesababisha kurudisha nyuma shughuli za maendeleo yao, kwa muda mrefu huku wakiiomba serikali kuhakikisha kero hizo zinatatuliwa kwa wakati.

Malalamiko hayo wametolewa leo katika mkutano wa hadhura ulioandaliwa na halmashauri hiyo na kufanyika katika stendi ya zamani ya mabasi mjini Nansio uliolenga wananchi kueleza kero na changamoto zinazowakabiri kwenye maeneo yao.

David Machumu, mmoja wa wananchi hao amesema kuwa, serikali wilayani humo inapaswa kuwaelimisha wananchi ambao wengi wao hawafahamu utaratibu wa masuala ya ardhi ili kuepukana na adha zinazowakabili.

“Pia kitengo cha ardhi kiboreshwe kwani kinaonekana hakipo makini na kuna upungu mkubwa,” amesema Machumu.

Machumu amesema pamoja na changamoto ya ardhi wananchi hao wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la maji safi na salama kwa muda mrefu hivyo serikali inapaswa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana.

George Nyamaha, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amemtaka Songoro Nyongo, Kaimu Mkurugenzi na Detius Burchardi, Kaimu Meneja Mradi wa Maji Safi na Mazingira (Mwauwasa) wawaeleze ukweli kuhusu tatizo maji na ardhi.

Pia, amewaagiza viongozi wanaowatumikia wananchi katika kata zao na mitaa, kufanya mikutano ya kubaini matatizo yanayowakabili wananchi na kuyapatia ufumbuzi ili kuisaidia halmashauri kutatua changamoto zilizopo.

Songoro amekiri halmashauri hiyo kukabiliwa na upungufu wa watumishi hususani kitengo cha ardhi kwa kutokuwa na ofisi ya ardhi kitendo kinachosababisha utendaji duni.

Burchardi amewaeleza wananchi hao kuwa, kuna tatizo katika mkondo mkubwa wa kuwapelekea maji kwenye tangi kubwa la Malegeya kuharibika na sasa matengenezo bado yanaendelea.

error: Content is protected !!