January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maji Ludewa yatengewa milioni 400/-

Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (kulia) akishiriki kujenga mradi wa maji kijiji cha Madindo Ludewa

Spread the love

SERIKALI imetenga Sh. 400 milioni kwa ajili ya uboteshaji wa miundombinu ya maji katika Mji wa Ludewa mkoani Njombe. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Pia serikali imesema kuwa, itaendelea kuboresha miundombinu ya maji katika mji wa Ludewa na viunga vyake kwa kadiri rasilimali fedha zitakavyopatikana.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kupeleka maji safi na salama katika Mji wa Ludewa.

Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema kwa mwaka wa fedha 2015/16 serikali imetenga Sh. 400 milioni.

Ameongeza kuwa, awali kwa mwaka wa fedha 2014/15, serikali ilitenga Sh. 500 milioni kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya maji katika mji huo.

Aidha, amesema serikali imetoa Sh. 100 milioni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji kutoka kwenye chanzo cha maji cha Mapetu ambapo taratibu za kumpata mkandarasi zimekamilika.

Kwa mujibu wa Majaliwa, mji wa Ludewa unakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 13,000 ambapo kati ya hao, asilimia 40 tu ndio wanaopata huduma ya maji kutoka kwenye vyanzo vya Ngalawale na Mkondachi.

error: Content is protected !!