Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maji chini ya ardhi ndio tegemeo – Mwinyi
Habari Mchanganyiko

Maji chini ya ardhi ndio tegemeo – Mwinyi

Bomba la maji safi
Spread the love

 

WAKATI mataifa kadhaa yanatumia raslimalifedha kubadilisha maji ya chumvi ili kupata maji ya matumizi ya nyumbani, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema tegemeo kubwa kwa Zanzibar litabakia kuwa la maji ya chini ya ardhi. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Rais Dk. Mwinyi amesema kuna haja kubwa na ya muhimu wataalamu kujenga mifumo itakayoihakikishia nchi kunufaika na vyanzo vya maji vilivyopo nchini kwa kuwa teknolojia ya ubadilishaji maji ya chumvi ni ya gharama kubwa.

Amesema hayo leo wakati akihutubia hadhara ya watu wapatao 300 wakiwemo wataalamu wa fani mbalimbali katika sekta ya maji wanaohudhuria Kongamano la kihistoria la maji.

Dk. Mwinyi alifungua kongamano hilo la siku mbili linalofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, mjini hapa likihusisha watafiti na wahandisi wa maji kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Maendeleo ya Sekta ya Maji Zanzibar.

“Kwa sababu sisi Zanzibar tunayo raslimali hii muhimu ya maji chini ya ardhi, ni muhimu sana kusimamia ulinzi na usalama wa vyanzo vya maji tulivyonavyo.

“… hivi na vingine vinavyotarajiwa kulingana na tafiti zinazofanyika sasa, ndio tegemeo la kupatikana kwa maji safi na salama kwa uhakika zaidi hapa kwetu Zanzibar,” alisema Rais Mwinyi huku akitambua tatizo linalokua la athari za kimazingira – mabadiliko ya tabianchi linaloikabili nchi.

Amesifu jitihada mpya zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar zikianzia na kuwakusanya wataalamu mbalimbali wa maji na washirika wa maendeleo na kufanikisha uzinduzi wa MpangoKazi wa Maendeleo ya Maji Zanzibar.

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Rais alizindua mpango huo Machi mwaka huu ambao ndio chimbuko la kongamano alolifungua leo likidhaminiwa na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

Amesema serikali inatambua mchango muhimu unaotolewa na washirika hao na kuahidi kuwa uongozi wake utaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kwa kuwa unachagiza mafanikio ya kupatikana kwa maji safi na salama ambayo ndiyo uhai wa binaadam na viumbe wengine wote.

Zanzibar imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa maji safi na salama kutokana na uchakavu wa miundombinu imara na mchango wa shughuli za utafiti katika sekta ya maji.

Akizungumzia maendeleo ya Sekta ya Maji Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa ZAWA, Dk. Salha Mohammed Kassim alisema kunatekelezwa miradi mikubwa mitatu kwa sasa ambayo ikikamilika kuanzia Desemba, itainua kiwango cha uhakika wa upatikanaji wa maji kufikia asilimia 82 kote Unguja na Pemba. Miradi hiyo ni pamoja na unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo wa Benki ya Exim ya India na ule wa ahueni ya UVIKO 19.

Washirika walioshirikiana na Wizara katika kuandaa na kufanikisha kongamano hilo lililotarajiwa kumalizika Alkhamis, ni pamoja na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA); Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji, Mafuta na Gesi (ZURA); Taasisi ya Uhandisi na Miundombinu ya Meil ya India; Chuo cha Maji Dar es Salaam; Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ); Vigor Zanzibar; Global Water Partnership Tanzania (GWP TZ); AFCONS Infrastructure Limited; Jumuiya ya Wataalamu wa Sayansi ya Bahari Ukanda wa Bahari ya Hindi (WIOMSA) na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!