August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majeshi Zanzibar matatani 

Spread the love

KAMBI rasmi ya upinzani Bungeni inalaani kitendo cha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutumia nguvu za kijeshi kutisha wananchi wa Zanzibar na kutumia mwanya huo kuchakachua mchakato wa kidemokrasia wa uchanguzi, anaandika Aisha Amran.

Juma Hamad msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wa wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, ameyasema hayo leo Bungeni wakati akiwasilisha maoni ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Amesema serikali itafakari upya matumizi sahihi ya Jeshi kulishirikisha katika mchakakato wa kutwaa madaraka ya dola kwa njia za ujanja ujanja ni hatari kubwa.

Hamad amesema kumezuka tabia ya watawala kulitumia Jeshi la Wananchi katika masuala ya ndani ya kisiasa ili kutimiza matakwa yao ya kisiasa kitendo ambacho kinadumaza demokrasia katika taifa.

 Ametoa mfano kinapofika kipindi cha uchaguzi, Zanzibar inakuwa kama vile nchi iliyovamiwa kijeshi (invaded country) vikosi vya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi, na Mgambo kutoka Tanzania bara vinapelekwa Zanzibar na kupiga makambi kwenye viwanja vya ndege, bandarini na kwenye vituo vya redio.

Aidha amesema vikosi hiyo vimekuwa vikipita mitaani na wakati mwingine kufanya mazoezi ya kijeshi katika maeneo ya makazi ya wananchi jambo ambalo huzua hofu kwa wananchi na kutoa taswira kama vile nchi inakabiliwa na vita.

Amesema wanatambua kwamba ulinzi wa raia na mali zao unafanywa na Jeshi la Polisi isipokuwa Jeshi la Ulinzi linaweza kuongeza nguvu ikiwa tu nchi iko vitani au kama hali ya hatari imetangazwa.

“Ni kwa nini Jeshi la Wananchi wa Tanzania likafanye kazi ya Jeshi la Polisi huko Zanzibar wakati Jeshi la Polisi lipo, nchi haipo vitani na pia hakuna hali ya hatari iliyotangazwa”.amesema Hamad.

“Ni vizuri demokrasia iachwe ichukue mkondo wake. Kwa maana hiyo, Jeshi libakie kulinda mipaka ya nchi yetu na kuilinda Serikali itakayowekwa madarakani na wananchi wenyewe”.amesema.

error: Content is protected !!